69. Ni ipi hukumu ya swalah ya mkazi nyuma ya msafiri au kinyume chake?

Swali 69: Ni ipi hukumu ya swalah ya mkazi nyuma ya msafiri au kinyume chake? Je, inafaa kwa msafiri kufupisha ni mamoja akiwa imamu au maamuma?

Jibu: Swalah ya msafiri nyuma ya mkazi na swalah ya mkazi nyuma ya msafiri zote mbili hazina neno. Lakini ikiwa maamuma ndiye huyo msafiri na imamu ndiye huyo mkazi, basi atalazimika kuswali kwa kukamilisha kwa sababu ya kumfuata imamu wake. Hilo ni kutokana na yale yaliyothibiti katika “Musnad” ya Imaam Ahmad na “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba aliulizwa juu ya swalah ya msafiri nyuma ya mkazi anayeswali Rak´ah nne ambapo akajibu kuwa hivo ndio Sunnah. Lakini mkazi akiswali nyuma ya msafiri katika swalah za Rak´ah nne basi atapaswa kukamilisha swalah yake pindi imamu atapotoa salamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 72-73
  • Imechapishwa: 13/09/2022