66. Mtume alimtambua ´Aaishah akiwa amevaa Niqaab

7 – ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi sallam) alipomtafakari Swafiyyah alimuona ´Aaishah kati ya watu wengine wote akiwa amevaa Niqaab ambapo akamtambua.”[1]

[1] Ibn Sa´d (8/90) ambaye amesema: al-Waliyd bin ´Atwaa’ bin al-Agharr al-Makkiy ametukhabarisha: Ibraahiym bin Sa´d ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Umar bin al-Khattwaab. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Wasimulizi wake ni wenye kuaminika na ni wanamme wa al-Bukhaariy na Muslim – wote isipokuwa huyu al-Waliyd. adh-Dhahabiy amemtaja katika “Miyzaan-ul-I´tidaal” na Ibn Hajar katika “Lisaan-ul-Miyzaan” na akasema:

”Ibn ´Adiy amemtaja na haikuwa inatakikana kwake kufanya hivo. Bwana huyo amefanywa kuwa ni mwaminifu.”

al-Waaqiydiy amepokea mfano wake. Lakini katika upokezi huo imekuja ya kwamba wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walifunika maumbo yao, lakini hakuna kinachofahamisha kuwa walikuwa wanalazimika kufanya hivo. Kwa ajili hiyo hakuna mgongano na yale maneno yaliyotangulia ya Haafidhw ya kwamba walikuwa wakionyesha miili yao, na si maumbo yao, mbele ya Maswahabah kutokana na haja au faida za kidini, jambo ambalo limeashiriwa katika maneno ya Haafidhw – na Allaah ndiye mjuzi zaidi. Ahmad (6/219) amepokea kutoka kwa Yaziyd bin Baabanuus ambaye amesema:

”Mimi na rafiki yangu tulienda kwa ´Aaishah na tukaomba idhini ya kuingia. Akaturushia mto na akajisitiri.”

Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 108-109
  • Imechapishwa: 08/10/2023