8 – Ibraahiym bin ´Abdir-Rahmaan bin ´Awf amesema:

”Wakati wa hajj yake ´Umar bin al-Khattwaab ya mwisho aliyohiji aliwaruhusu wakeze Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pamoja na ´Uthmaan bin ´Affaan na ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf. ´Uthmaan alikuwa akiita kwa sauti: ”Zindukeni! Hairuhusu kwa yeyote kuwakaribia! Hairuhusiwi kwa yeyote kuwatazama!”Walikuwa wamekaa juu ya mikoba yao juu ya ngamia. Wanaposhuka chini, basi wanashushwa kwenye njia ya mlima na huku ´Uthmaan na ´Abdur-Rahmaan walikuwa chini ya njia ya mlima. Hakuna yeyote aliyepanda mahali walipo.”[1]

[1] Ameipokea al-Bayhaqiy (7/93) kupitia kwa Sa´daan bin Naswr: Sufyaan bin ´Uyaynah ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaswim al-Ahwal. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh. Sa´daan jina lake ni Sa´iyd ambaye mara nyingi anatambulika kama Sa´daan, kama alivosema al-Khatwiyb katika “Taariykh Baghdaad”. ad-Daaraqutwniy na wengine wamemzingatia kama mwenye kuaminika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 08/10/2023