Uombezi kwa anayemswalia Mtume kwa wingi

Swali: Anayemswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa wingi ni miongoni mwa watu wenye haki zaidi ya kupata uombezi wake?

Jibu: Ni kwa wote. Muhimu ni kuingia Peponi. Uombezi mkubwa utawakusanya wote makafiri na waislamu. Ni kuhusiana na uombezi ili wahukumiwe kati yao. Lakini nyombezi zingine zinahusu mizani kuwa mizito, thawabu kubwa, kuingia Peponi na kusalimika kutokana na Moto. Hizo ni nyombezi zingine. Ataombea nyombezi nyingi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kukiwemo wakazi wa Motoni katika wale watenda madhambi.

Jibu: Uombezi huu ni maalum kwa yule mwenye kumswalia Mtume?

Jibu: Ndio, ambaye ni muislamu. Kuhusu kafiri matendo yake ni yenye kuharibika kukiwemo kumsifu kwake na mengineyo:

وَلَوْ أَشْرَكُوا لَحَبِطَ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ

“Lau wangemshirikisha bila shaka yangeporomoka yale waliyokuwa wakitenda.”[1]

Hautomfaa kitu kutokana na shirki.

[1] 06:88

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23007/ما-الشفاعة-الخاصة-باصحاب-الصلاة-والتسليم
  • Imechapishwa: 08/10/2023