65. Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka wa 10?

Swali 65: Ni misafara ipi ya kijeshi ilifanyika mwaka wa 10?

Jibu: Khaalid bin al-Waliyd alitumwa katika msafara wa kijeshi kwenda Najraan. Mwanzoni mwa mwezi wa Dhul-Qa’dah akaja na kabila zima wakiwa waislamu.

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamtuma ´Aliy kwenda Yemen kabla ya hijjah ya kuaga. Baadaye akarudi na vile vichinjwa vya Hadiy.

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akamtuma Abu Muusa al-Ash´ariy na Mu´aadh bin Jabal kwenda Yemen kuwa wakala nchini humo. Akawaamrisha wafanye wepesi na wasitie uzito, waeneza bishara njema na wasikimbize, washirikiane na wasigawanyike.

Hijjah ya kuaga ilifanyika katika mwaka huu. Hapo zikawa zimekamilika nguzo za Uislamu.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 131
  • Imechapishwa: 01/11/2023