Wasia juu ya kutumia wakati katika mambo yenye faida

Mtu mwenye busara ni yule mwenye kukubali wasia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ambaye anapupia juu ya yale yenye kumnufaisha. Ni wingi uliyoje wa wale wenye kutumia wakati wao katika mambo yasiyokuwa na faida! Bali wanatumia wakati wao katika mambo yaliyo na madhara juu ya nafsi zao na dini yao. Kwa ajili hii tunawaambia watu hawa kuwa hawakutendea kazi wasia wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanafanya hivo ima kwa kutokujua au kwa kupuuza. Lakini hata hivyo muumini mwenye busara ni yule anayekubali wasia kama huu na anapupia juu ya yale mambo yenye kumnufaisha katika dini na dunia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/78-79)
  • Imechapishwa: 01/11/2023