Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Pindi mja anapoacha kutendea kazi matendo yaliyowekwa katika Shari´ah katika baadhi ya mambo yake, hupungua hamu yake ya mambo yaliyowekwa katika Shari´ah na kunufaika nayo kwa kile kiwangoalichozowea upande mwingine. Hilo ni tofauti na yule mtu ambaye hima yake ni kwa yale mambo yaliyowekwa katika Shari´ah. Mapenzi yake juu ya mambo yaliyowekwa katika Shari´ah ni makubwa na ananufaika nayo pakubwa; anaitimiza dini na kukamilisha Uislamu wake. Kwa ajili hiyo utamuona mtu ambaye anasikiliza sana qaswiydah kwa ajiliya kutaka kuutengeneza moyo wake hupungua shauku yake ya kusikiliza Qur-aan mpaka ikafikia huenda akaichukia. Ambaye anasafiri kwa wingi kwenda katika makaburi na sehemu zingine mfano wake, hakubaki moyoni mwake mapenzi na matukuzo ya kuhiji nyumba Tukufu kama vile yule ambaye moyo wake umekunjuka kwa Sunnah. Ambaye amezowea kuchukua hekima na adabukutoka katika maneno ya wahenga wa wafursi na warumi, basi hukosa sehemu ya hekima na adabu za Kiislamu mfano wake. Yule ambaye amezowea kusoma visa na historia za wafalme, basi hukosa visa na historia za Mitume mfano wake na kadhalika. Kwa ajili hiyo Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inasema:

“Hakuna watu wanaozua Bid´ah, isipokuwa Allaah huondoa sehemu katika Sunnah mfano wake.”[1][2]

Ameipokea Imaam Ahmad.

[1] Ahmad (4/105). Cheni ya wapokezi ni dhaifu.

[2] Iqtidhwaa’-us-Swiraatw al-Mustaqiym (1/483-484). Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah pia amesema:

”Wakati mioyo zinapokula Bid´ah, basi hakubaki nafasi yoyote ya Sunnah. Inafanana na yule anayekula chakula kibaya.” (Iqtidhwaa’-us-Swiraatw al-Mustaqiym (02/597-598)).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 24/05/2023