50. Hapa ndipo huzuka mifumo ya ulinganizi ya kizushi

Waislamu wanadogeka na kudhoofika pale ambapo mifumo ya kizushi ndio inakuwa yenye kusheheni kati yao, kwa sababu njia hizo hazitoki isipokuwa kutoka kwa watu wenye ´Aqiydah iliyopinda, imani dhaifu na iliochafuliwa kwa Bid´ah. Mifumo hii ya kizushi hutumika pale ambapo kunadhoofika kushikamana na mapokezi ya kinabii. Kwa sababu “kila ambavyo Ummah unadhoofika kushikamana na fimbo ya Manabii wao na kila ambavyo imani yao inadhoofika, ndivo wanavyopata badala yake Bid´ah na shirki”[1]. Wakati nyoyo zinafungamana na Bid´ah hizi, ndivyo zinazuiwa kutokamana na Sunnah. Matokeo yake hazioni katika Sunnah yale wanayoyaona ndani ya yale yaliyozuliwa. Kwa ajili hiyo ndio maana wakaipa mgongo Sunnah. Hassaan bin ´Atwiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Hakuna watu waliozusha Bid´ah ndani ya dini yao, isipokuwa Allaah huondoa sehemu katika Sunnah mfano wake kisha haiwarudilii tena mpaka siku ya Qiyaamah.”[2]

[1] Ighaathat-ul-Lahfaan (1/200).

[2] ad-Daarimiy kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Kumepokelewa mfano wake kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) na kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ijapo haikusihi.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 70
  • Imechapishwa: 24/05/2023