Swali 48: Ni vita vipi vilitokea mwaka wa nne?

Jibu: Vita vya Banuun-Nadhwiyr ambavyo vilisababisha kufukuzwa na ngawira bila kupigana vita. Suurah “al-Hashr” ikateremshwa kuhusiana na hilo. Katika mwaka huohuo, katika mwezi wa Rabiy’ al-Awwal, ikaharamishwa pombe.

Kuna maoni mengine yasiyokuwa na nguvu yanayosema kuwa vita hivyo vilitokea Dhaat-ur-Riqaa´ mwaka huohuo Jumaadaa al-Uulaa, lakini maoni yenye nguvu yanasema kuwa vilitokea mwaka wa saba baada ya Khaybar.

Katika mwaka huohuo waislamu wakaenda Badr kwa mara ya pili baada ya kutishiwa na Abu Sufyaan. Hata hivyo Abu Sufyaan hakutokea katika vita hivyo.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 112-113
  • Imechapishwa: 14/10/2023