77. Mtazamo wa Salaf kuhusu nguo zenye kuonyesha

Umm ´Alqamah bin Abiy ´Alqamah amesema:

”Nilimuona Hafswah bint ´Abdir-Rahmaan bin Abiy Bakr akiingia kwa ´Aaishah. Alikuwa amevaa shungi jembamba inayoonyesha kifua chake. ´Aaishah akairarua na kusema: ”Je, hivi wewe hujui aliyoteremsha Allaah katika Suurah ”an-Nuur”? Kisha baada ya hapo akaitisha mtandio na kumvisha.”[1]

Hishaam bin ´Urwah amesema:

”Wakati al-Mundhir bin az-Zubayr alipofika kutoka ´Iraaq alimtumia Asmaa´ bint Abiy Bakr vitambaa vyembamba na vizuri baada ya kupoteza macho yake. Akavipapasa vitambaa vile kwa mkono wake na kusema: ”Ah. Mrudishie vitambaa vyake.” Akachukulia vibaya na kusema: ”Ee mama! Havionyeshi kwa ndani.” Asmaa´ akasema: ”Hata kama havionyeshi kwa ndani vinaonyesha maumbo.”[2]

´Abdullaah bin Abiy Salamah amesema:

”´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh) aliwapa wanamme vitambaa vya coptic kisha akasema: ”Msiwaache wanawake wenu wakavishonea kanzu.” Bwana mmoja akasema: ”Ee Kiongozi wa waumini! Nimemwacha mwanamke wangu amekivaa. Ameenda huku na huku nyumbani na sijaona kuwa vinaonyesha kwa ndani.” ´Umar akasema: ”Hata kama havionyeshi kwa ndani vinaonyesha maumbo.”[3]

Mapokezi haya yanaashiria kuwa mavazi ambayo ima yanaonyesha ndani au yanaonyesha maumbo hayajuzu, na kwamba mavazi yanayoonyesha ndani ni mabaya zaidi kuliko mavazi yanayoelezea maumbo. Ndio maana ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) akasema:

”Shungi ni ile ambayo inafunika ngozi na nywele.”[4]

Shumaysah amesema:

”Niliingia kwa ´Aiashah na alikuwa amevaa nguo nene, shuka ya juu, shungi na sketi iliokuwa imepakwa rangi ya manjano.”[5]

[1] Ibn Sa´d (8/46): Khaalid bin Makhlad ametuhadithia: Sulaymaan bin Bilaal ametuhadithia, kutoka kwa ´Alqamah bin Abiy ´Alqamah, kutoka kwa mama yake.

[2] Ibn Sa´d (8/184) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kwenda mpaka kwa al-Mundhir.

[3] al-Bayhaqiy (2/234-235) aliyesema kuwa cheni ya wapokezi imekatika. Bi maana kati ya ´Abdullaah bin Abiy Salamah na ´Umar. Lakini wasimulizi wake ni wenye kuaminika na inatiliwa nguvu na maneno ya al-Bayhaqiy:

” Muslim al-Butwayn pia ameipokea kutoka kwa Abu Swaalih kutoka kwa ´Umar.

[4] al-Bayhaqiy (2/235) aliyesimulia kwa cheni ya wapokezi pungufu na akasema:

”Tumesimuliwa kuwa ´Aaishah aliulizwa kuhusu mtandio ambapo akasema: ”Shungi ni ile ambayo inafunika ngozi na nywele.”

[5] Ibn Sa´d (8/70) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh kwenda mpaka kwa Shumaysah bint ´Aziyz bin ´Aamir al-´Atakiyyah al-Baswriyyah. Haafidhw Ibn Hajar amesema juu yake:

”Ni mwenye kukubaliwa.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 126-129
  • Imechapishwa: 15/10/2023