78. Nguo zinazoonyesha ndani ya mwili ni dhambi kubwa

Kwa ajili hiyo wanazuoni wamesema:

”Ni wajibu kufunika uchi kwa njia ya kwamba ngozi isionekane… Nguo ni lazima iwe ya kitambaa kinene au cha ngozi. Akijifunika kwa nguo nyembamba ambayo inaonyesha rangi ya ngozi haijuzu, kwa sababu sitara haifikiwi kwa nguo kama hiyo.”[1]

Ibn Hajar al-Haytamiy ameandika mlango mzima kuhusu nguo nyembamba ya mwanamke inayoonyesha mwili na akathibitisha kuwa ni miongoni mwa madhambi mkubwa. Amenukuu Hadiyth zilizotangulia kisha akasema:

”Dhambi hii kujumuishwa miongoni mwa madhambi makubwa ni jambo liko wazi, kwa sababu kumekuja matishio makali juu yake. Sijamuona aliyeyatamka hayo waziwazi, isipokuwa yale yaliyosemwa kwamba ni kujifananisha na wanamme, jambo ambalo haliwezi kuwa na haki zaidi.”

Hadiyth zinazowalaani wanawake wanaojifananisha na wanamme zitatajwa wakati tutapozungumzia sharti ya sita.

[1] al-Muhadhdhab (3/170) kwa maelezo ya ”al-Majmuu´”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 129
  • Imechapishwa: 15/10/2023