Swali: Kuna kaburi la mchanga na linakanyagwa kwa miguu. Je, inafaa kuweka kizuizi juu ya kaburi hilo kwa ajili ya kulilinda na kufungwa kwa chandarau?

Jibu: Inafaa kuyafungia makaburi – ni mamoja makaburi hayo ni mengi au machache – kwa wavu au kitu kingine ikiwa malengo ni kuyahifadhi yasije kutwezwa na sio kwa ajili ya kuyatukuza au kuchupa mpaka kwayo. Ama kulifungia wavu kaburi maalum au kulijengea ni kitu kisichojuzu. Kwa sababu kufanya hivo ni kuchupa mpaka kwalo. Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa amekataza kulitia chokaa kaburi, kukaa juu yake na kujenga juu yake[1]. Kama ambavo imethibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamab amewalaani wenye kuyafanya makaburi kuwa ni mahali pa kuswalia[2].

Kuhusu kitendo cha kupanda juu yake miti hakijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum) hawakufanya jambo hilo. Sababu nyingine kitendo hicho ni aina fulani ya kuchupa mpaka. Kuna khatari watu wakapewa mtihani kwa ile miti inayomea juu yake.

Kuhusiana na kitendo cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupanda makuti mawili juu ya makaburi ya wale watu wawili waliokuwa wakiadhibiwa, maoni sahihi zaidi ya wanazuoni ni kwamba jambo hilo ni maalum kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa makaburi hayo mawili peke yake. Kwa sababu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya hivo kwa makaburi yaliyosalia. Vivyo hivyo Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum). Hivyo basi ikatambulika kuwa jambo hilo ni maalum kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwa watu hao wa makaburi mawili peke yao. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mjuzi zaidi.

wa as-Salaam ´alaykum wa Rahmatullaahi wa Barakaatuh.

[1] Muslim (970).

[2] al-Bukhaariy (436) na Muslim (529).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 142-143
  • Imechapishwa: 27/07/2022