Kisa cha uwongo kuhusu uchengukwaji wa wudhuu´ kwa nyama ya ngamia

Swali: Rafiki yangu mmoja amenambia kuwa kisa cha hukumu ya kuchenguka wudhuu´ kwa kula nyama ya ngamia ni kwamba kulikuweko jopo lililokuwa limekaa pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambapo akapatwa mmoja wao na hadathi. Kwa hiyo ili Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aweze kumsitiri ndipo akasema:

”Yeyote aliyekula nyama ya ngamia basi na atawadhe.”

Ndipo kikosi cha watu wale wakasimama na kutawadha. Je, kisa hiki ni sahihi? Je, kutawadha kwa ajili ya kula nyama ya ngamia ni lazima au inapendekeza tu?

Jibu: Kisa hicho ni batili. Hakina mlolongo wa wapokezi. Ni batili miongoni mwa batili. Kuna maoni matatu:

1 – Amri ya kutawadha iliyofutwa. Ni batili.

2 – Amri kwa njia ya mapendekezo na sio ya ulazima. Imekaribiana na hiyo ya  kwanza.

3 – Amri katika mlango wake kwa njia ya ulazima. Hivo ndivo wanavoonelea Hanaabilah na Muhaddithuun.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 119
  • Imechapishwa: 01/07/2022