49. Kulihamisha kaburi mahali pengine kwa ajili ya kuepusha shari

Swali: Baba yangu alifariki nikiwa bado mdogo ambapo akazikwa katika makaburi ya ami yangu. Baada ya kupita miaka kadhaa kukatokea mzozo kati yangu mimi na ami yangu ambapo akanambia nimwondoshe baba yangu kwenye makaburi yake na akanitishia kunifanyia mambo mabaya endapo sintofanya hivo. Sikuwa na namna isipokuwa kuitikia maombi yake na nikahamisha mwili wa baba yangu kwenda katika makaburi yanayonihusu. Je, napata dhambi kwa kufanya hivo? Je, makaburi ni milki ya waliohai ambapo wanaweza kufanya wakatavyo au ni milki ya wakazi wake?

Jibu: Kumhamisha baba yako kutoka makaburi moja kwenda makaburi mengine kwa ajili ya kuepusha shari na mtihani hakuna neno kwako na wala si vibaya kufanya hivo na himdi zote njema anastahiki Allaah.

Kuhusu makaburi inategemea. Ikiwa yule aliyeyatenga aliyakusudia watu maalum, basi wengine hawana ruhusa ya kuzikwa maeneo hapo isipokuwa kwa idhini yake. Ikiwa ameyatenga kwa ajili ya ndugu jamaa zake, majirani zake au kabila fulani, basi wengine hawana ruhusa ya kuzikwa maeneo hapo isipokuwa kwa idhini yake. Lakini ikiwa alikusudia waislamu wote kwa jumla au kwa ajili yake, majirani zake, jamaa zake na waislamu, basi hakuna kizuizi akazikwa kila muislamu katika jamaa zake na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr min Fitnat-il-Qubuur, uk. 143-144
  • Imechapishwa: 27/07/2022