275 – ´Aliy bin Ibraahiym amenihadithia: Ya´quub bin Muhammad ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz bin Abiy Haazim ametuhadithia:

”Ilifika jioni moja ´Aaishah akiwa amefunga. Hakuna na kitu isipokuwa mikate miwili ya bapa. Akaja mwombaji, ambapo akaamrisha apewe mkate ule. Baadaye akaja mwingine, ambapo akaamrisha apewe ule mkate mwingine. Mjakazi wake akakataa na kusema: ”Tazama utafuturu kwa kitu gani.” Wakati jua lilipozama, mtu mmoja akabisha hodi. ´Aaishah akasema: ”Ni nani?” Wakasema: ”Mjumbe wa fulani.” ´Aaishah akasema: ”Ikiwa ni mtumwa mwache aingie ndani.” Tahamaki akaingia na nyama ya kondoo iliyochomwa iliokuwa na mkate. Ndipo ´Aaishah akamwambia kijakazi yule: [Tupu] Hii ni kwa ajili ya ile mikate ya bapa. Naapa kwa Allaah! Hawakunipa chochote katika hayo.”

276 – Haaruuun bin Sufyaan ametuhadithia: al-Mu´aytwiy ametuhadithia: Baqiyyah ametuhadithia: Abu ´Abdillaah bin Salaam al-Wihaadhwiy ametuhadithia:

”Mtu mmoja ambaye alihudhuria kwa khaliyfah al-Waliyd bin Yaziyd amenihadithia kwamba mtoto wake alikuwa anakula chakula cha mchana pamoja naye. Akawa anatafuna tonge kwa kulizungusha huku na kule, ambapo akasema: ”Ole wako! Liteme. Kwani ni ngumu zaidi kwenye tumbo lako kuliko ulimi wako.”

277 – Haaruun bin Sufyaan ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr al-Mu´aytwiy ametuhadithia: Baqiyyah ametuhadithia: Artwaah bin al-Mundhir amenihadithia, kutoka kwa Dhwamrah bin Habiyb, ambaye amesema:

”Kundi la madaktari lilikusanyika kwa mfalme mmoja miongoni mwa wafalme. Akawauliza ni ipi dawa kuu ya tumbo. Kila mmoja akasema ya kwake. Bwana mmoja akanyamaza. Walipomaliza, akamwambia: “Wewe unasemaje?” Akasema: ”Kila mmoja amesema mambo ambayo yanaweza kuwa na baadhi ya manufaa. Lakini yote hayo yanaweza kufupishwa kwenye mambo matatu: usile chakula kabisa isipokuwa pale ambapo unalazimika kukila, usile nyama mpaka iwe nyororo na kuiva vizuri na wala usimeze tonge isipokuwa baada ya kulitafuna sana, ili tumbo lisipambane nalo.”

278 – Haaruun bin Sufyaan ametuhadithia: al-Aswma´iy ametuhadithia: ´Amr bin Hudhwaym amenihadithia:

”Nilimuona Sufyaan ath-Thawriy akinunua nyama huko Makkah kwa sehemu ya kumi na mbili ya sarafu ya fedha.”

279 – Haaruun amenihadithia: al-Aswma´iy amenihadithia:

”Nimefikiwa na khabari kuwa Sufyaan ath-Thawriy alikuwa akitengeneza mikate miwili ya bapa kwa ajili ya chakula chake cha mchana na cha jioni. Akija mwombaji, basi humpa nusu ya mkate. Akija mwombaji mwingine baada ya hapo, anasema: ”Allaah akukunjulieni!”

280 – Haaruun amenihadithia: al-Aswma´iy amenihadithia: Abu ´Amr bin al-´Alaa’ amenihadithia:

”Ikiwa mtu amekaa kwenye safuria yake, akawakaribisha majirani na familia yake.” Bwana mmoja akamwambia: ”Kwenye safuria yake?” Akasema: ”Hapana, lakini nyinyi hammimini maji.”

281 – Ahmad bin ´Uthmaan bin Hakiym al-Awdiy ametuhadithia: al-Husayn bin ´Aliy, mpwa wa Layth, ametuhadithia: ´Abdullaah bin az-Zubayr ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin Shariyk, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

”Wakati ´Aliy alipomuoa Umm-ul-Baniyn bint Haazim, aliikaa naye muda wa siku saba. Katika ile siku ya saba alijiliwa na kundi la wanawake, ambapo ´Aliy akampa Qanbar dirhamu moja na kusema: ”Wanunulie zabibu.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 165-169
  • Imechapishwa: 06/08/2023