282 – Muhammad bin ´Uthmaan al-´Ijliy amenihadithia: Khaalid bin Makhlad ametuhadithia: ´Abdullaah bin ´Umar ametuhadithia, kutoka kwa Naafiy´, kutoka kwa Ibn ´Umar, kutoka kwa ´Umar, ambaye amesema:

”Jihadharini na nyama. Kwani hakika inaleta ukali kama pombe.”

283 – Muhammad bin Bakr bin Khaalid ametuhadithia: al-Fudhwayl bin ´Iyaadh ametuhadithia, kutoka kwa Hishaam bin Hassaan, kutoka kwa Hishaam bin ´Urwah, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Aaishah, aliyesema:

”Nyumba ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wanaweza kukutana na miezi mitatu bila ya kutengeneza mkate.”

284 – Muhammad bin al-Mughiyrah amenihadithia: Kathiyr bin Hishaam ametuhadithia: Yahyaa ametuhadithia, kutoka kwa Matwar al-Warraaq, aliyesema:

”Mmoja katika Mitume wa Allaah alimlalamikia Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) unyonge wake, ambapo Allaah akamwamrisha apike nyama kwa maziwa.”

285 – Ya´quub bin ´Ubayd amenihadithia: Yaziyd bin Haaruuun ametukhabarisha: Ja´far bin Burd ametukhabarisha: Umm Saalim ar-Raasibiyyah ametuhadithia, kutoka kwa ´Aaishah, aliyesema:

”Alikuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anapoletewa maziwa, husema: ”Ni wangapi wako nyumbani? Baraka moja au mbili.”[1]

286 – Ibraahiym bin Sa´iyd amenihadithia: ar-Rabiy´ bin Naafiy´ ametuhadithia: Ismaa´iyl bin ´Ayyaash ametuhadithia, kutoka kwa Shurahbiyl bin Muslim, ambaye amesema:

”´Uthmaan bin ´Affaan alikuwa akiwatengenezea watu chakula cha wakuu, ambapo anaingia nyumbani kwake akila siki na mafuta.”

287 – Haaruun bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia: ´Ubaydullaah bin Shumaytw ametuhadithia: Nilimsikia Shumaytw bin ´Ajlaan akisema: Nimemsikia al-Hasan akisema:

”Yakini ya muumini ni yenye kubadilika. Kinamtosha kile kinachomtosha mbuzi mdogo; konzi moja ya tende na glasi ya maji.”

288 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: Qurrah bin ´Abdir-Rahmaan ametuhadithia, kutoka kwa az-Zuhriy, kutoka kwa ´Urwah, kutoka kwa Asmaa’:

”Wakati alipokuwa anapika uji, anaufunika mpaka unaacha kuvuta na akisema: ”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: ”Ndio kina baridi zaidi.”[2]

289 – Muhammad bin Hassaan as-Samatwiy ametuhadithia: ´Aliy bin ´Aabis ametuhadithia, kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Abu Raziyn, ambaye amesema:

”Abu Waa-il kwenye karamu yake ya ndoa alialika kichwa cha ng´ombe na mikate minne ya bapa.”

[1] Ibn Maajah (3321). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah” (660).

[2] Ahmad (6/350) na al-Haakim (4/118), aliyeisahihisha kwa mujibu wa sharti za Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “as-Swahiyhah” (659).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 169-173
  • Imechapishwa: 06/08/2023