49. Unanunua kila unachokitamani?

290 – Muhammad bin ´Abbaad bin Muusa amenihadithia: Zayd bin al-Habbaab ametukhabarisha: Abu Ka´b muuza hariri amenikhabarsha: Anas bin Siyriyn ametukhabarisha:

”´Abdullaah bin ´Umar alitamani samaki safi, ambapo waliletwa samaki wa kucomwa kutoka maili kadhaa kutoka Madiynah. Kisha akafanyiwa mkate laini. Wakati wa kukata swawm, akaletewa nao kwenye sahani. Akawatazama na kusema: ”Wapeleke kwa watoto mayatima wa fulani.” Mwanamke wake akamwambia: ”Kula angalau kile kitachokuondoshea tamaa yako, kisha baadaye tutawapeleka kwa watoto mayatima wa fulani.” Akasema: ”Wapeleke kwa watoto mayatima wa fulani. Wakijiondoshea tamaa yako basi tamaa yangu pia itakuwa imeondoka.” Nikakariri matakwa yangu na yeye akakariri jibu lake.”

291 – Muhammad bin ´Abbaad ametuhadithia: Zayd bin al-Habbaab ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Umar, kutoka kwa Swaalih bin Kaysaan, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah, amabye amesema:

”´Umar alimuona na nyama, aliyokuwa ameinunua kwa dirhamu moja. Akainua juu bakora yake, ambapo akasema: ”Ee Kiongozi wa waumini, sikuinunua kwa ajili yangu. Baadhi ya familia yangu wametamani nyama, ndipo nikawanunulia.” Ndipo akamwacha.”

292 – Muhammad bin ´Abbaad ametuhadithia: Zayd bin al-Habbaab ametuhadithia, kutoka kwa [tupu] Abu Muhammad, ambaye amesema:

”al-Hasan alialikwa kwenye karamu ya ndoa. Tukaenda naye. Watu wakala na yeye akala na akawaombea du´aa ya baraka.” Kukaambiwa: ”Wameleta chakula hiki na hiki, kuliko kile kingine.” Akasema: ”Hakuna ubadhirifu katika chakula.”

293 – Muhammad bin ´Abbaad amenihadithia: Zayd bin al-Habbaab ametuhadithia, kutoka kwa Abu Bakr al-Baswriy: Yuunus bin ´Ubayd ametukhabarisha:

”Wakati tulipokuwa kwa al-Hasan, alipewa zawadi ya kikapu cha sukari. Akafungua kikapu kile na akaona aina nzuri kabisa ya sukari. Akaonyesha kwa mguu wake tuchukue, yaano tule.”

294 – ´Aliy bin al-Hasan bin Abiy Maryam amenihadithia, kutoka kwa Yahyaa bin Ishaaq: Hazm al-Qutwa´iy ametuhadithia:

”Maalik bin Diynaar alikuwa anatamani samaki kwa muda mrefu, akamwambia mmoja katika ndugu zake: ”Nilikuwa natamani samaki kwa kipindi kirefu.” Akamwandalia kisha akamletea. Akashika ndevu zake kisha akasema: ”Ee Maalik! Unakula kila ambacho unakitamani? Utajipatishia kila unachokitaka? Ni ubaya uliyoje unayofanya, ee Maalik! Aibu kwako! Umefanya vibaya, ee Maalik!”

295 – Ibn Abiy Maryam amenihadithia, kutoka kwa Hajjaaj bin Nuswayr: al-Mundhir Abu Yahyaa ametuhadithia:

”Nilimuona Maalik bin Diynaar akiwa na mguu wa wanyama hawa waliopikwa. Akamnusa kitambo, mpaka akapitiwa na mzee aliyepewa mtihani. Hivyo akampa mguu ule, akapangusa kwa mkono wake ukutani, akaweka vazi lake kwenye kichwa na kuondoka zake. Akakutana na mmoja katika marafiki zake akasema: ”Hii leo nimeona kwa Abu Yahyaa jambo la kushangaza.” Akasema: ”Kitu gani hicho?” Akamweleza yaliyopitika. Ndipo akasema: ”Naweza kukueleza kuwa alikuwa anamtamani kwa kitambo kirefu. Hakuwa anahisi furaha kumla, akamtoa swadaka.”

296 – Haaruun bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sayyaar ametuhadithia: ´Uthmaan bin Ibraahiym, mmoja katika marafiki zake Maalik bin Diynaar, ametuhadithia:

”Nilimsikia Maalik akimwambia mmoja katika marafiki zake: ”Mimi natamani mkate laini na mkate mzito kwa mtindi.” Bwana yule akaondoka na kumletea navyo. Akawa anavitazama kisha akasema: ”Nilikuwa nakutamani kwa kipindi cha miaka arobaini na nikikushinda – je, unataka kunishinda hii leo? Viondoshe kutoka kwangu.” Akakataa kuvila.”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 173-177
  • Imechapishwa: 06/08/2023