46. Sababu ya walimwengu wote kumwabudu Allaah pekee

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Kila kisichokuwa Allaah ni walimwengu [kimeumbwa] na mimi ni mmoja katika walimwengu hao.

MAELEZO

Kisha Shaykh (Rahimahu Allaah) akabainisha namna alivyotumia Aayah iliopita.

Kila kisichokuwa Allaah ni walimwengu – Hivyo Allaah ndiye anakuwa Mola. Kwa sababu Allaah ndiye Mola wa walimwengu na mimi ni mmoja katika walimwengu hao. Kwa hiyo Allaah ndiye anakuwa Mola. Kwa hiyo hakuna yeyote awezaye kusema kuwa Yeye yuko na Mola mbali na yule Mola wa walimwengu. Ni mamoja kafiri wala muislamu. Hili ni jambo lisilowezekana kabisa. Haya hayasemwi na mtu mwenye akili. Hii ni dalili juu ya uola wa Allaah (´Azza wa Jall). Midhali Yeye ndiye Mola wa walimwengu basi Yeye ndiye ambaye anastahiki kuabudiwa. Jambo hili linabatilisha ´ibaadah ya asiyekuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa ajili hiyo amesema baada yake:

إِيَّاكَ نَعْبُدُ وَإِيَّاكَ نَسْتَعِينُ

“Wewe pekee ndiye tunakuabudu na Wewe pekee ndiye tunakuomba msaada.”[1]

Hili linafidisha ufupikaji. Kwa sababu kutangulizwa kwa kitendo na kucheleweshwa kwa mtendaji kunafahamisha ufupikaji. Kusema Wewe pekee ndiye tunakuabudu ni tofauti na tunakuabudu. Kwa sababu kusema “tunakuabudu” ni kuthibitisha peke yake. Lakini “Wewe pekee ndiye tunakuabudu” ndani yake kuna ukanushaji na uthibitishaji. Kwa msemo mwingine ni kwamba hatumwabudu mwengine asiyekuwa Yeye. ´Ibaadah haisihi isipokuwa pamoja na ukanushaji na uthibitishaji. Hiyo ndio maana ya hapana mungu isipokuwa Allaah. Ndani yake mna ukanushaji na uthibitishaji. Ndani yake kunakanushwa kufanyiwa ´ibaadah mwengine asiyekuwa Allaah na wakati huohuo anathibitishiwa nayo Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 01:05

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 101
  • Imechapishwa: 16/12/2020