45. Dalili ya kwamba Allaah ndiye Mola anayestahiki kuabudiwa na walimwengu wote

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

MAELEZO

Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”[2]

Aayah hii ndio Aayah ya kwanza ndani ya msahafu. Kabla yake hakuna isipokuwa Basmalah. Isitoshe ndio maneno ya mwisho ya watu wa Peponi. Amesema (Ta´ala):

وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Na wito wao wa mwisho ni: himdi zote njema zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu.”[3]

Allaah alianza kuwaumba viumbe kwayo. Amesema (Ta´ala):

الْحَمْدُ لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَجَعَلَ الظُّلُمَاتِ وَالنُّورَ

“Himdi zote njema zinamstahikia Allaah ambaye ameumba mbingu na ardhi na akajaalia viza na nuru.”[4]

Akamaliza kuwaumba viumbe kwayo. Amesema (Ta´ala):

وَقُضِيَ بَيْنَهُم بِالْحَقِّ وَقِيلَ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Itahukumiwa baina yao kwa haki na itasemwa: himdi zote njema zinamstahikia Allaah, Mola wa walimwengu.”[5]

Ameanza na akamaliza kuwaumba viumbe kwayo. Kwa hiyo ni maneno matukufu.

Himdi – Ni sifa kwa yule muhimidiwa pamoja na kumpenda na kumtukuza. Maana yake ni kwamba sifa zote njema ni stahiki ya Allaah. Yeye ndiye anastahiki sifa kamilifu. Kuhusu wengine wanatakiwa kushukuriwa kwa kiasi cha ule wema waliyofanya. Ama sifa njema kamilifu ni kwa Allaah  (´Azza wa Jall). Kwa sababu neema zote ni kutokana na Yeye.

Hata viumbe wanapokufanyia kitu katika wema kimetokana na Allaah (´Azza wa Jall). Yeye ndiye amemwepesisha kiumbe huyu juu yako na kummanikisha akufanyie wema. Kwa hiyo himdi zinarejea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Himdi zote njema ni zenye kuthibiti kwa Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 01:02

[2] 01:02

[3] 10:10

[4] 06:01

[5] 39:75

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 98-100
  • Imechapishwa: 16/12/2020