Pindi nilikuwa Dameski Shaam na nilikuwa nikihojiana na baadhi ya Hizbiyyuun kama vile al-Ikhwaan al-Muslimuun na Hizb-ut-Tahriyr, walikuwa wakinambia:

”Hivi wewe unafanya kitu gani? Hakuna kundi lolote pembezoni mwako. Hakuna vijana wowote pembezoni mwako. Kazi yako tu ni kusoma vitabu vya kale.”

Nilikuwa nikiwaambia kwa adabu zote kwamba mimi ni mwalimu wa masomo. Nini anachofanya mwalimu wa Qur-aan? Anafunza Qur-aan. Mimi natekeleza wajibu huu. Nini mnachotaka nifanye? Hakuna ninachoweza kufanya zaidi ya hicho. Mnataka niachane na kitendo hichi na niishi bila malengo au niendelee na kazi yangu? Wananyamaza na hawana la kusema. Nitaendelea na kazi yangu. Kama nyote mnavojua kazi hii imeleta matunda mazuri katika ulimwengu wa Kiislamu na himdi zote anastahiki Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1010)
  • Imechapishwa: 16/12/2020