41. Huyu ndiye ambaye anatafuta njia mpya za kulingania

Zingatia, ee mwenye akili, maneno haya na yatazame kwa jicho la uadulifu ili uone namna ambavo Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum) walikemea kila mfumo ambao haukupokelewa kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – hata kama njia hiyo ni yenye manufaa, inaulainisha moyo,inamvutia mpotevu katika haki na mfano wake. Tunasema kwa kukata kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametubainishia kila kitu. Laiti ingelikuwa njia hizi zinawanufaisha waja basi Shari´ahi singeziacha; ingeziamrisha, ima maamrisho ya ulazima au maamrisho ya mapendekezo.

Muumini pekee ambaye anatukuza njia ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na anaona kuwa imekamilika ndiye ambaye anayakubali maneno haya na anajisalimisha kwayo. Ama ambaye ameihusisha nafsi yake kwa kitu kingine ndiye ambaye hutafuta njia mpya ili kuikamilisha Shari´ah na kuikamilisha dini. Hakika sisi ni wa Allaah na Kwake ndiko tutarejea! Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ وَمَن يُطِعِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَخْشَ اللَّـهَ وَيَتَّقْهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ

“Hakika si vyenginevyo kauli ya waumini wanapoitwa kwa Allaah na Mtume wake ili awahakumu kati yao, basi husema: “Tumesikia na tumetii” – na hao ndio wenye kufaulu. Na yeyote yule atakayemtii Allaah na Mtume wake na akamuogopa Allaah na akamcha, basi hao ndio wenye kufuzu.”[1]

وَمَن يَعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا

“Anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika amepotoka upotofu wa wazi.”[2]

وَذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا إِلَىٰ مَا أَنزَلَ اللَّـهُ وَإِلَى الرَّسُولِ رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودً

“Wanapoambiwa: “Njooni kwenye yale aliyoyateremsha Allaah na kwa Mtume”, basi utawaona wanafiki wanakugeukilia mbali kwa mkengeuko.”[3]

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.”[4]

[1] 24:51-52

[2] 33:36

[3] 4:61

[4] 4:65

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 50-51
  • Imechapishwa: 22/05/2023