Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka, Ahl-us-Sunnah na Salafiyyuun

Swali: Je, ni kweli kuwa unatofautisha kati ya kundi lililonusuriwa na kundi lililookoka?

Jibu: Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka. Ni moja.

Swali: Huyatofautishi kati yake?

Jibu: Ni moja.

Swali: X jana jioni alikuwa na muhadhara na akasema kuwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz anaafikiana naye juu ya hilo.

Jibu: Hapana, hapana. Kundi lililonusuriwa ndio kundi lililookoka na wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Wao ni Ahl-us-Sunnah, kundi lililookoka na kundi lililonusuriwa.

Swali: Na wao ni Salafiyyuun?

Jibu: Na wao ni Salafiyyuun. Wao ni kundi lililookoka kwa sababu wameokoka kutokana na Moto, wao ni kundi lililonusuriwa kwa sababu wameahidiwa kunusuriwa na wao ni Ahl-us-Sunnah kwa sababu wanazifuata Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=9jJcabonJGM&app=desktop
  • Imechapishwa: 21/05/2023