Ibn Baaz kuhusu harakati za al-Ikhwaan al-Muslimuun

Swali: al-Ikhwaan al-Muslimuun wameingia Saudi Arabia tangu kipindi fulani. Wamekuwa ni wenye uchangamfu kati ya wanafunzi. Unasemaje juu ya harakati hizi na ni kiasi gani imeafikiana na mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah?

Jibu: al-Ikhwaan al-Muslimuun wamekosolewa na wanazuoni wakubwa kwa kuwa hawatilii umuhimu kulingania katika Tawhiyd na kukemea shirki na Bid´ah. Wana njia maalum ambazo nafasi zake zinafanya kutolingania kwa Allaah na ´Aqiydah sahihi walionayo Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. al-Ikhwaan al-Muslimuun wanatakiwa kutilia umuhimu wa kulingania kwa mujibu wa ulinganizi wa Salafiyyah na kulingania kwa Allaah na kukataza kuyaabudia makaburi, kuwategemea wafu, kuwataka msaada wafu kama al-Husayan, al-Badawiy au wengine. Wanatakiwa kutilia umuhimu msingi huu mkuu, nayo ni maana ya  ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah` ambayo ndio msingi wa dini. Kitu cha kwanza ambacho Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwalingania wakazi wa Makkah ni kumpwekesha Allaah na maana ya ´hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah`.

Wanazuoni wengi wanawakosoa al-Ikhwaan al-Muslimuun kwa sababu ya jambo hili. Hawatilii mkazo kulingania kuabudiwa kwa Allaah pekee na kutakasiwa Yeye ´ibaadah na kukemea yale yaliyozuliwa na wajinga pindi wanapowategemea wafu na kuwataka msaada, kuwawekea nadhiri na kuchinja kwa ajili yao, mambo ambayo ndio shirki kubwa.

Jengine wanalowakosoa ni kutoitilia umuhimu kuifuata Sunnah, kuzipa umuhimu Hadiyth tukufu na yale waliyokuwemo Salaf katika hukumu mbalimbali za Shari´ah.

Kuna mambo mengine mengi. Nasikia mengi ambayo al-Ikhwaan wanakosolewa kwayo. Tunamuomba Allaah awaongoze.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: (al-Majallah (Toleo la 806, uk. 24, 1416-02-25))
  • Imechapishwa: 21/05/2023