41. Hadiyth ”Yule mwenye kuacha kuniswalia… “

41 – Ismaa´iyl bin Abiy Uways ametuhadithia: Sulaymaan bin Bilaal ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من ينسى الصلاة عليَّ خطئ أبواب الجنة

”Yule mwenye kuacha kuniswalia, basi atapotea kutokamana na milango ya Pepo.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi wake ni nzuri, lakini kuna Swahabah anayekosekana.  Ja´far anaitwa Ja´far bin Muhammad bin ´Aliy bin al-Husayn bin ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anhum). Baba yake Muhamamd anajulikana kama Abu Ja´far al-Baaqir. Mtunzi wa kitabu ataipokea kupitia njia mbili zitazokuja huko mbele kutoka kwake, lakini hali ya kukosekana Swahabah. Hata hivyo  at-Twabaraaniy ameiunganisha katika “al-Mu´jam al-Kabiyr” (1/139/1) kupitia kwa Muhammad bin Bashiyr al-Kindiy: ´Ubaydah bin Humayd ametuhadithia: Fitwr bin Khaliyfah amenihadithia, kutoka kwa Abu Ja´far Muhammad bin ´Aliy bin al-Husayn, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa baba yake, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema… Kwa mujibu wa ad-Daaraqutwniy al-Kindiy si mwenye nguvu katika masimulizi yake, kwa ajili hiyo hakuzingatiwi kule kukhalifu kwake. Pengine ndio maana al-Mundhiriy akasema kuwa kuwa Hadiyth inafanana zaidi na ambayo kuna Swahabah aliyekosekana katika cheni ya wapokezi. Hata hivyo Hadiyth inatiliwa nguvu na upokezi wa Ibn ´Abbaas kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ameipokea Ibn Maajah (908) na upokezi wa Muhammad bin al-Hanafiyyah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ibn Abiy ´Aaswim ameipokea hali ya kukosekana Swahabah katika cheni ya wapokezi. Hata kama njia zote hizi zina udhaifu, lakini zinapeana nguvu. Kwa ajili hiyo Hadiyth angalau kwa uchache kabisa ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 46-47
  • Imechapishwa: 16/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy