42. Hadiyth ”Atakayeacha kuniswalia… ”

42 – ´Aliy bin ´Abdillaah ametuhadithia: Sufyaan ametuhadithia: ´Amr amesema, kutoka kwa Muhammad bin ´Aliy bin Husayn, ambaye amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من ينسى الصلاة [عليَّ] خطئ طريق الجنة

”Atakayeacha kuniswalia, basi atapotea njia ya Peponi.”[1]

Sufyaan amesema: Bwana mmoja, pamoja na ´Amr, amesema: Nimemsikia Muhamamd bin ´Aliy akisema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من ذكرت عنده فلم يصل عليَّ خطئ طريق الجنة

”Ambaye nitatajwa mbele yake na asiniswalie, basi atapotea njia ya Peponi.”

Kisha Sufyaan akamtaja bwana mmoja huyo; Bassaam as-Swayrafiy.

[1] Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh, lakini kuna Swahabah anayekosekana. Hapa kuna ufuatiliaji wenye nguvu kabisa wa Ja´far bin Muhammad, kutoka kwa ´Amr bin Diynaar, ambao umesimiliwa na Sufyaan bin ´Uyaynah. Mwanzoni hakumtaja bwana ambaye ameipokea kutoka kwa Muhammad bin ´Aliy, kisha baadaye akamtaja kama Bassaam, ambaye ni Ibn ´Abdillaah as-Swayrafiy, naye ni mwaminifu.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 47
  • Imechapishwa: 16/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy