40. Kijakazi anatakiwa kuvaa kama mwanamke wa kiungwana

Ibn Sa´d ametukhabarisha: Muhammad bin ´Umar ametukhabarisha, kutoka kwa Ibn Abiy Sabrah, kutoka kwa Abu Sakhr, kutoka Ibn Ka´b al-Quradhwiy ambaye amesema:

”Kuna mnafiki mmoja alikuwa akiwanyanyasa wanawake wa kiumini akiwaudhi. Kila anapoambiwa basi hutoa udhuru kwamba alikuwa anafikiri kuwa ni wajakazi. Ndipo Allaah akawaamrisha wavae kwa kujitofautisha na wajakazi na badala yake wajiteremshie jilbaab zao.”[1]

Upokezi huu si Swahiyh bali ni dhaifu mno kutokana na sababu zifuatazo:

1 – Muhammad bin Ka´b al-Quradhwiy ni mwanafunzi wa Maswahabah na hakuwahi kukutana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa hivyo kuna Maswahabah wanaokosekana katika cheni ya wapokezi.

2 – Ibn Abiy Sabrah, ambaye jina lake anaitwa Abu Bakr bin ´Abdillaah bin Muhammad bin Abiy Sabrah, alikuwa ni dhaifu mno. Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Ametuhumiwa kuunda.”[2]

3 – Muhammad bin ´Umar, naye ni al-Waaqidiy, alikuwa anatambulika kuwa mnyonge. Bali alikuwa mwenye kutuhumiwa.

Ibn Jariyr na as-Suyuutwiy[3] wamepokea mfano wa mapokezi kama haya, lakini mapokezi yote hayo kuna Maswahabah wanakosekana katika cheni za wapokezi na hazisihi. Kwa sababu zinaishilia kwa Abu Maalik, Abu Swaalih, al-Kalbiy, Mu´aawiyah bin Qurrah na al-Hasan al-Baswriy. Hakukuja cheni yoyote iliyoungana na kwa ajili hiyo hazijengewi hoja, khaswa kwa kuzingatia kwamba udhahiri wake unapingana na Shari´ah na akili. Kwa sababu maana ya mapokezi hayo ni kwamba wajakazi wa Kiislamu – na kati yao walikuweko wajakazi wa Kiislamu – waliacha kujisitiri na wala hakuwaamrisha jambo hilo ili kuepukana na maudhi ya watenda maasi. Jambo la kushangaza ni kuona namna ambavyo baadhi ya wafasiri wa Qur-aan wanavyodanganyika na mapokezi haya dhaifu na hivyo wakasema kuwa maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ

”… na wanawake wa waumini… ”

inawakusudia wale wanawake waungwana na si wale wajakazi. Wakajengea juu ya hilo kwamba haiwalazimu wanawake waungwana kufunika kichwa na nywele. Bali baadhi ya madhehebu wameenda mbali zaidi wakasema kuwa uchi wa kijakazi ni kama uchi wa mwanammke; kuanzia kwenye kitovu mpaka kwenye magoti. Wakasema kuwa inafaa kwa wanamme wa kando kutazama nywele za kijakazi, mikono, miguu, kifua na matiti yake[4]. Haya, licha ya kwamba hayana dalili kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah, yanapingana na ueneaji wa maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ

”… na wanawake wa waumini… ”

Ni kwa njia ya kuenea kama yalivyo maneno Yake Allaah (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا ۚ وَإِن كُنتُم مَّرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا صَعِيدًا طَيِّبًا فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُمْ

“Enyi walioamini! Msikaribie swalah na hali mmelewa mpaka mjue kile mnachokisema na wala mkiwa mna janaba isipokuwa mmo safarini mpaka muoge josho na mkiwa wagonjwa au safarini au mmoja wenu ametoka msalani au mmewagusa [kuwajamii] wanawake kisha hamkupata maji, basi fanye Tayammum kwa ardhi safi ya mchanga – pakeni nyuso zenu na mikono yenu.”[5]

Kwa ajili hiyo Abu Hayyaan al-Andalusiy amesema:

”Udhahiri ni kuwa maneno Yake:

وَنِسَاء الْمُؤْمِنِينَ

”… na wanawake wa waumini… ”

yanakusanya waungwana na wajakazi. Mtihani wa wajakazi ni mkubwa zaidi kuliko wanawake waungwana. Kwa hivyo kunahitajika dalili ya wazi inayowatoa nje ya ueneaji wa wanawake.”[6]

Haafidhw Ibn-ul-Qattwaan[7] na wengineo wamekwishatangulia katika mkondo huohuo.

[1] at-Twabaqaat al-Kubraa (8/176).

[2] at-Taqriyb.

[3] Tazama “ad-Durr al-Manthuur”.

[4] Ahkaam-ul-Qur-aan (3/390) ya Abu Bakr al-Jassaas.

[5] 4:43

[6] al-Bahr al-Muhiytw (7/250).

[7] Tazama “Ahkaam-ul-Qur-aan” (2/24 – muswada).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 90-92
  • Imechapishwa: 20/09/2023