Aidha Allaah (Ta´ala) amebainisha hekima ya amri ya kujiteremshia jilbaab pale aliposema:

ذَلِكَ أَدْنَى أَن يُعْرَفْنَ فَلَا يُؤْذَيْنَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَّحِيمًا

”Hivyo kunapeleka karibu zaidi watambulikane wasiudhiwe. Na Allaah daima ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Kwa msemo mwingine ni kwamba, pindi mwanamke anapojiteremshia jilbaab basi anatambulika kuwa ni katika wake wenye kujichunga na machafu, wasafi na wazuri. Hivyo haudhiwi na wale watenda madhambi. Hilo ni tofauti na pale anapotoka hali ya kuwa amevaa vibaya na kutojisitiri. Watenda madhambi wanakuwa na matumaini kwa wanawake kama hao ambapo wanawasumbua na kuwanyanyasa, jambo ambalo linashuhudiwa katika kila zama na kila wakati. Kwa ajili hiyo Allaah (Ta´ala) akawaamrisha wanawake wote wa kiumini kujisitiri, kwa ajili ya kufunga upenyo huo.

[1] 33:59

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 90
  • Imechapishwa: 20/09/2023