38. Katika hali hii haifai kwa mwanamke kuonyesha uso na mikono yake

Hata hivyo tunatakiwa kuzindua kwamba inafaa kwa mwanamke kuonyesha uso na mikono yake ikiwa hakutia kitu chochote kile katika mapambo. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَهُنَّ

”Wasidhihirishe mapambo yao.”[1]

Vinginevyo atalazimika kufunika viwili hivyo. Hilo khaswa hii leo ambapo wanawake wamebobea katika kuzipamba nyuso na mikono yao kwa aina mbalimbali za mapambo na rangi. Hakuna mwanamme yeyote mwenye wivu, sembuse muislamu, anayetilia shaka juu ya uharamu wake. Uharamu huo haujumuishi wanja na hina kwa sababu vimevuliwa katika Aayah, kama ilivyotangulia. Ibn Sa´d amepokea kutoka kwa Sufyaan, kutoka kwa Mansuur, kutoka kwa Rib´iy bin Khuraash, kutoka kwa dada yake na Hudhayfah (ambaye alikuwa na dada zake waliokutana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)) ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutolea Khutbah akasema: ”Enyi kongamano la wanawake! Je, nyinyi hamna fedha mnazojipamba? Kwani hakuna mwanamke yeyote ambaye anajipamba kwa dhahabu na akazionyesha isipokuwa ataadhibiwa kwazo.” Mansuur akasema: ”Nikamweleza hayo Mujaahid ambaye akasema: ”Nimekutana na wanawake hao. Mmoja wao alikuwa anaweza kufunika pete kwa mkono wake.”[2]

Kujengea kwangu hoja hakuko katika Hadiyth hii inayotamka waziwazi iliyosimuliwa na mwanamke asiyemtambulika; kujengea kwangu hoja ni katika maneno ya Mujaahid ambayo ni andiko la wazi linalosapoti yale niliyotaja. Kisha nimeyapata maneno ya Mujaahid yamepokelewa kwa cheni nyingine ya wapokezi katika ”al-Musnad” ya Abu Ya´laa.

[1] 24:31

[2] at-Twabaqaat al-Kubraa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 89-90
  • Imechapishwa: 20/09/2023