Fawziy al-Ashariy amesema:

“Imaam Ishaaq (Rahimahu Allaa) amesema:

“Imani ni matendo na vitendo. Inazidi na kushuka na inashuka mpaka hakubaki chochote.”

Ameipokea al-Khallaal katika “as-Sunnah”[1] kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Imaam Ishaaq bin Mansuur ameafikiana na Ishaaq (Rahimahu Allaah) na akasema:

“Nami nasema hivo.”

Amelitaja hilo katika “al-Masaa-iyl” yake”[2].”[3]

Cheni ya wapokezi ni dhaifu. Kwa sababu yumo Muhammad bin Haazim ambaye hatambuliki. Sikupata wasifu wake. Nadhani kuwa huyu al-Ashariy anajua jambo hilo.

Isitoshe miongoni mwa mambo yanayoshangaza ya al-Bahrayniy huyu ni kwamba ameona matamshi mawili moja kwa moja kabla ya maneno ya Ishaaq:

1 – Ameyapokea al-Khallaal kupitia kwa Ismaa´iyl ambaye amesema:

“Nilimuuliza Ahmad kuhusu mtu mwenye kusema kuwa imani inazidi na kushuka ambapo akajibu: “Huyu yuko mbali na Irjaa´.”[4]

2 – al-Khallaal amesema: Abu Bakr al-Marruudhiy ametukhabarisha, ´Abdul-Malik al-Maymuuniy, Abu Daawuud as-Sijistaaniy, Harb bin Ismaa´iyl al-Karmaaniy, Yuusuf bin Muusa, Muhammad bin Ahmad bin Waaswil na al-Hasan bin Muhammad na wote wamesema kuwa wamemsikia Ahmad bin Hanbal akisema:

“Imani ni maneno na matendo, inazidi na kushuka.”[5]

Matamshi haya mawili hayakumshtua mpumbavu huyu kutokana na kung´ang´ania maneno ya Ishaaq ambayo hayakuthibiti kutoka kwake. Imaam Ahmad amezungumza maneno ambayo Maswahabah na wale walowafuata kwa wema wameafikiana juu yake. Huyu ni mwenye kujidhulumu mwenyewe wakati anapowapuuza na kunukuu kutoka kwa Ishaaq maneno ambayo hayakuthibiti kutoka kwake ili kuwapachika nayo wapinzani wake Rabiy´ na ndugu zake kuwa ni Murji-ah. Hajali jambo hilo ingawa hukumu yake inaweza kuwarejelea Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale waliowafuata kwa wema.

Je, mwenendo huu juu ya maneno ya wanazuoni haufahamishi kuwa bwana huyu ni katika Ahl-ul-Ahwaa´? Anachukua yale yanayoafikiana na matamanio yake, pasi na kujali matokeo yake na athari yake, na anayaficha yale yanayoenda kinyume na matamanio yake, ijapo yatakuwa yamefahamishwa na maafikiano na Qur-aan na Sunnah.

[1] 3/582.

[2] 2/589.

[3] al-Burkaan, uk. 9-10.

[4] as-Sunnah (3/581).

[5] as-Sunnah (3/582).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 87
  • Imechapishwa: 20/09/2023