1 – Mimi nilikuwa miongoni mwa wa mwanzo wanaopiga vita ya kwamba matendo ni sharti ya kukamilika kwa imani (شرط الكمال) au kwamba ni sharti ya kusihi kwa imani (شرط الصحة). Niliendelea kukemea jambo hilo miaka kadhaa mpaka hii leo.

2 – Nilisema na bado nasema kuwa imani inaweza kushuka mpaka kusibaki chochote. Nimesema hivo na mfano wake. Hata hivyo sijui kama kuna yeyote katika waliotangulia na wale waliokuja baadaye ambaye amesema kuwa ni sharti wakati wa kuitambulisha imani. Hakuna waliosema hivo isipokuwa tu Haddaadiyyah ambao imewajaa chuki dhidi ya Ahl-us-Sunnah.

Jambo hilo linapelekea kuwazingaatia Salaf wote kuwa wapotevu. Hata wale Salaf waliosema kuwa imani inashuka hadi hakubaki chochote mara nyingi huishilia kusema kuwa imani ni maneno na vitendo na inazidi na kushuka. Hawasema jengine zaidi ya hivo. Wengine husema kuwa imani ni maneno na matendo na hawazidishi hapo, kama alivyoyanukuu hayo al-Bukhaariy kutoka kwa zaidi ya 1000 ya waalimu zake.

3 – Mimi sipingi ziada inayosema “mpaka hakubaki chochote” na wala simkaripii anayesema hivo. Maneno yake Fawziy al-Bahrayniy juu yangu:

“Kuhusu kupinga kwake tamko linalosema “Imani inashuka mpaka hakubaki chochote”…”

ni katika uwongo wake. Nimetamka tamko hilo katika darsa ambayo walihudhuria mamia ya wanafunzi katika Ahl-us-Sunnah.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 86
  • Imechapishwa: 20/09/2023