Swali 24: Ni wakati gani ulivunjika mkataba?

Jibu: Kwa muda wa miaka mitatu walikuwa wamezingirwa katika kifungu. Hatimaye Hishaam bin ´Amr, Zuhayr bin Abiy Umayyah, Mutw´im bin ´Adiy, Abul-Bakhtariy bin Hishaam na Zam´ah bin al-Aswad bin ´Abdil-Muttwalib wakaona wafute mkataba huo. Ukapasuliwapasuliwa ambapo mchwa ukala vile vipandevipande vyote isipokuwa tu jina la Allaah (´Azza wa Jall). Aliyaeleza hayo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kabla ya kuchanwa kwake[1].

[1] Tazama ”as-Siyrah” (1/430) ya Ibn Hishaam, al-Bukhaariy (3882) na (1589), ”as-Siyrah”, uk. 221 ya adh-Dhahabiy na ”al-Fusuul”, uk. 66-67 ya Ibn Kathiyr.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 20/09/2023