39. Tofauti ya المدح na الْحَمْد

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ

”Himdi zote njema ni za Allaah.”[1]

Hili ni kwa wingi na linakusanya himidi zote.

Kuhusu uzuri ambao mtu hana taathira juu yake, kama mfano wa urembo na mfano wake, kusifiwa kwayo kunaitwa matapo (المدح) na sio himdi.

MAELEZO

Himdi ni kule kumsifu mwenye kuhimidiwa kwa sifa zake anazo taathira juu yake. Hili ni kamilifu zaidi kuliko matapo (المدح).

Maneno yake:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ

”Himdi zote njema ni za Allaah.”

Hili ni kwa wingi na linakusanya himidi zote. Ukisema hivo maana yake ni kwamba himdi zote njema ni Zako, ee Allaah. Kwa msemo mwingine aina zote za himdi anazistahiki Allaah.

Maneno yake:

“Kuhusu uzuri ambao mtu hana taathira juu yake, kama mfano wa urembo na mfano wake, kusifiwa kwayo kunaitwa matapo (المدح) na sio himdi. Himdi ni kule kumsifu yule msifiwaji kwa sifa zake anazo taathira juu yake. Kwa msemo mwingine ni kwamba unamsifu kwa zile sifa anazofanya kwa kutaka kwake mwenyewe. Ni kama mfano wa pale anaposifiwa mtu ya kwamba ni mkarimu, mwenye kutoa sana au shujaa. Lakini ukimsifu kuwa ni mrefu au kwamba ni mweupe sana. Sifa hizi hana taathira juu yake. Kitendo hichi huitwa matapo. Pindi unapomsifu mwenye kusifiwa kwa sifa ambazo hana taathira kwazo huitwa matapo. Unapomsifu kwa sifa ambazo ana taathira kwazo hutwa himdi. Kumsifu mwenye kusifiwa kwa sifa zake yuko na taathira kwazo ndio kukamilifu zaidi, kwa sababu anazifanya kwa kutaka kwake mwenyewe. Kwa ajili hii akasema (Ta´ala):

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”

Hakusema:

أمدح لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Matapo yote ni ya Allaah, Mola wa walimwengu.”

[1] 01:02

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 66-68
  • Imechapishwa: 13/06/2022