38. Ulazima wa kusoma al-Faatihah ipasavyo katika kila Rak´ah

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

al-Faatihah ni Aayah saba. Ya kwanza yake ni:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”[1]

Aaya ya sita:

صِرَاطَ الَّذِينَ أَنْعَمْتَ عَلَيْهِمْ

“Njia ya wale Uliowaneemesha… “

Aayah ya saba:

غَيْرِ الْمَغْضُوبِ عَلَيْهِمْ وَلَا الضَّالِّينَ

“… si ya walioghadhibikiwa wala waliopotea.”[2]

Kwa maana nyingine ni kwamba ni Aayah saba pasi na Basmalah kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanachuoni[3]. Hayo yanafahamishwa na maandiko. Moja wapo ni yale aliyopokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Allaah (Ta´ala) amesema:

“Nimeigawanya swalah kati Yangu Mimi na mja wangu mafungu mawili na mja Wangu atapata kile anachoomba. Mja akisema:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”

Allaah (Ta´ala) husema:

“Amenihimidi mja Wangu…. “[4]

Maneno yake:

“Nimeigawanya swalah kati Yangu Mimi na mja wangu mafungu mawili.”

Makusudio ya “swalah” ni al-Faatihah. al-Faatihah ina majina mengi na miongoni mwayo ni ´swalah`.

Maneno yake:

Mja akisema:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”

Allaah (Ta´ala) husema:

“Amenihimidi mja Wangu…. “

yanafahamisha kuwa Aayah ya kwanza ni:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”

Kama Basmalah ingelikuwa ni sehemu katika al-Faatihah basi Mola angesema:

Mja akisema:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”[5]

Kama ingelikuwa ni sehemu katika al-Faatihah, basi ingelibatilika swalah ya baadhi ya maimamu kwa sababu ya kutokusoma kwao Basmalah katika Rak´ah ya pili.  Wakati mwingine unawaona baadhi ya watu wanaposimama katika Rak´ah ya pili wanasema:

“Allaahu Akbar:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”

Kule kudondosha kwake Aayah kunaibatilisha swalah yake kujengea juu ya maoni yanayosema kuwa ni Aayah ya kwanza katika al-Faatihah. Lakini maoni ya sawa ni kwamba sio sehemu katika al-Faatihah. Hakika si venginevyo Aayah ya kwanza ni:

الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ

”Himdi zote njema ni za Allaah, Mola wa walimwengu.”

Ni lazima kusoma al-Faatihah. Nayo ni Aayah saba. Haitakiwi kudondosha herufi yake hata moja. Mtu akidondosha herufi yake hata moja basi swalah inabatilika.

Vivyo hivyo zile herufi ambazo zinatakiwa kukazwa kwa herufi mbili. Ndani ya al-Faatihah zipo herufi za kukazia (شَدَّة) kumi na moja ambazo ni lazima kwa mtu kuzileta.

[1] 01:02

[2] 01:07

[3] Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (22/277, 440).

[4]Muslim (395).

[5] 01:01

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 65-66
  • Imechapishwa: 13/06/2022