37. Mapendekezo ya kuleta Basmalah mwanzoni mwa kila Suurah

Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”[1]

Baraka na kuomba msaada.

MAELEZO

Maneno yake:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”

Kwa (الباء) maana yake ni kuomba msaada kwa jina la Allaah.

Maana ya:

“Baraka na kuomba msaada.”

ni kwamba natafuta baraka kwa kutaja jina la Allaah na naomba msaada kwalo katika mambo.

الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

“Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”

Ni majina Yake mawili (Ta´ala) yanayoenda sambamba; moja wapo ni nyepesi  zaidi kuliko lingine.

Basmalah ni kule kusema:

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيم

”Kwa jina la Allaah, Mwingi wa kurehemu, Mwenye kurehemu.”

Ni jambo limesuniwa ndani ya swalah mwanzoni mwa al-Faatihah na mwanzoni mwa kila Suurah isipokuwa Suurah “al-Baraa´”. Ni jambo limependekezwa kama mfano wa kuomba ulinzi.

Maoni ya sawa ni kwamba Basmalah ni Aayah yenye kujitegemea mwanzoni mwa kila Suurah. Sio sehemu ya Suurah. Sio sehemu katika al-Faatihah wala Suurah nyingine.

[1] 01:01

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 64-65
  • Imechapishwa: 13/06/2022