Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

رَبِّ الْعَالَمِينَ

“Mola wa walimwengu.”[1]

Mola ni Mwabudiwa, Muumba, Mwenye kuruzuku, Mfalme, Anayevisimamia na kuvilea viumbe vyote kwa neema Zake.

الْعَالَمِينَ

“… walimwengu.”

Ni kila kisichokuwa Allaah. Naye ni Mola wa walimwengu.

MAELEZO

Yeye (Subhaanah) amewalea viumbe wote – waumini na makafiri – kwa neema Zake. Anawalea waja Wake waumini malezi maalum. Anawalea kwa kule kumwabudu Kwake Yeye (Subhaanah), kumtii Kwake kwa kutaka kwao wenyewe, wanampwekesha kwa ´ibaadah na anawaongoza.

Wale wote wasiokuwa Allaah ni walimwengu. Watu ni walimwengu, majini ni walimwengu, Malaika ni walimwengu, ndege ni walimwengu, wadudu ni walimwengu, wanyama ni walimwengu, mbingu ni walimwengu, ardhi ni walimwengu na bahari ni walimwengu. Kila kisichokuwa Allaah ni walimwengu.

Yeye ndiye Mola wa walimwengu wote hawa. Yeye ndiye kaviumbe na anaviendesha. Walimwengu wote wako chini ya mkamato wa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 01:02

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 69
  • Imechapishwa: 13/06/2022