Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

“Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”[1]

Mwingi wa huruma ni huruma unaowapata viumbe wote.

Mwenye kurehemu ni huruma maalum kwa waumini. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَكَانَ بِالْمُؤْمِنِينَ رَحِيمًا

“Naye daima ni Mwenye kuwarehemu waumini.”[2]

MAELEZO

Mwingi wa huruma wanaingia waumini na makafiri. Miongoni mwa rehema za Allaah (Ta´ala) kwa makafiri ni pamoja na Yeye kuwaumba, kuwapa chakula, kuwanywesha, kuwaruzuku na kuwapa muda licha ya kwamba ni makafiri.

Allaah ni mwenye kuwarehemu waumini rehema maalum ambapo akawangoza, akawawafikisha kwa imani na akawasamehe.

الرَّحْمنِ الرَّحِيمِ

“Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu.”

Haya ni majina mawili ya Allaah (´Azza wa Jall).

[1] 01:02

[2] 33:43

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 70
  • Imechapishwa: 13/06/2022