Kuna aina mbili ya majina ya Allaah:

1 – Kuna sampuli ambayo ni maalum kwa Allaah na haifai kwa mwengine kujiita nayo. Mfano wa majina hayo ni Allaah. Hili ndio jina tukufu zaidi la Allaah ambalo haifai akajiita nalo mwengine.  Vivyo hivyo Mwingi wa rehema (ar-Rahmaan) haiwezekani kwa yeyote akajiita ar-Rahmaan. Vilevile Mola wa walimwegu, Mfalme wa wafalme, Muumba wa viumbe, Mwenye kunufaisha, Mwenye kudhuru, Mwenye kutoa (al-Mu´twiy), Mwenye kuzuia (al-Maaniy´), Mwenye kukamata (al-Qabdhw), Mwenye kukunjua (al-Baasitw), Mwenye kushusha (al-Khaafidhw) na Mwenye kunyanyua (ar-Raafiy´).

2 – Kuna sampuli ambayo ni majina ambayo Allaah anashirikiana kuitwa nayo na viumbe. Mfano wa majina hayo ni (Mwenye huruma) ar-Rahiym. Hili ni jina shirikishi. Anaitwa nalo Allaah na wengineo. Amesema (Ta´ala) kuhusu Mtume wake:

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

”Hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe. Yanamuhuzunisha yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni na kwa waliomuamini ni mpole na mwenye huruma.”[1]

Amemsifu Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ni mwenye huruma. Mengine ni kama Mwenye nguvu asiyeshindika (al-´Aziyz), Muweza (al-Qadiyr), Mwenye kusikia na Mwenye kuona.

Kila jina miongoni mwa majina ya Allaah kunatolewa ndani yake sifa. Sio majina matupu. Bali yamebeba sifa. Mwingi wa huruma (ar-Rahiym) limebeba sifa ya huruma. Mjuzi wa kila kitu (´Aliym) limebeba sifa ya ujuzi. Muweza (Qadiyr) limebeba sifa ya uwezo. Mwenye kusikia kila kitu (as-Samiy´) limebeba sifa ya usikizi. Mwenye kuona kila kitu (al-Baswiyr) limebeba sifa ya kuona. Mwenye hekima (al-Hakiym) limebeba sifa ya hekima. Mtukufu (al-´Adhwiym) limebeba sifa ya utukufu na mengineyo.

[1] 09:128

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 70-71
  • Imechapishwa: 13/06/2022