37. Ulinganizi kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah

Kundi jingine linalisema kuwa mlinganizi anatakiwa kulingania kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah peke yake, na si halali kwa yeyote kuingiza kitu ambacho hakukuidhinishwa na Allaah. Kwa msemo mwingine inatakiwa iwe kwa mfumo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Haya ndio maoni ya haki yanayotiliwa nguvu na Qur-aan na Sunnah na matendo ya Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Maoni hayo yamejengeka juu ya nukta tatu:

1 – Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ameikamilisha dini na ameitimiza neema Yake kwa waja Wake:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.”[1]

Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yeyote atakayezua ndani ya Ummah huu kitu chochote ambacho hakikufanywa na watangu wao, basi atakuwa amedai kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekhini dini. Kwa sababu Allaah (Ta´ala) amesema:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.” [2]

2 – Allaah (Ta´ala) amewajibisha kumtii Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akafungamanisha kufaulu kwa mja kwa utiifu huo, na amekataza kumuasi na akafungamanisha kula khasara kwa mja kwa kumuasi:

وَمَن يُطِعِ اللّهَ وَالرَّسُولَ فَأُوْلَئِكَ مَعَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللّهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ وَالصِّدِّيقِينَ وَالشُّهَدَاء وَالصَّالِحِينَ وَحَسُنَ أُولَئِكَ رَفِيقًا

“Atakayemtii Allaah na Mtume basi hao watakuwa pamoja na wale Allaah aliowaneemesha – Manabii na wakweli na mashahidi na waja wema – na uzuri ulioje kuwa na tangamano kama hili!”[3]

وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَإِنَّ لَهُ نَارَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا

“Yeyote atakayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi hakika atapata Moto wa Jahannam hali ya kudumu humo milele.”[4]

3 – Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kila kheri na akakataza kila shari, akahalalisha vilivyo vizuri na akaharamisha vilivyo vibaya. Allaah (Ta´ala) amesema wakati alipokuwa akimweleza:

فَالَّذِينَ آمَنُوا بِهِ وَعَزَّرُوهُ وَنَصَرُوهُ وَاتَّبَعُوا النُّورَ الَّذِي أُنزِلَ مَعَهُ ۙ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Basi wale waliomuamini na wakamtukuza na wakamnusuru na wakafuata nuru iliyoteremshwa pamoja naye, hao ndio wenye kufaulu.”[5]

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ صِرَاطِ اللَّـهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِلَى اللَّـهِ تَصِيرُ الْأُمُورُ

”Na hivyo ndivyo tulivyokuletea Roho katika amri Yetu. Hukuwa unaelewa nini Kitabu na wala imani, lakini tumeijaalia kuwa ni nuru, tunamwongoza kwayo Tumtakaye kati ya waja Wetu. Na hakika wewe bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka – Njia ya Allaah ambaye ni Vyake pekee vyote vilivyomo mbinguni na vyote vilivyomo ardhini. Tanabahi! [Kuwa ni] kwa Allaah pekee yanaishia mambo yote.”[6]

Abu Dharr (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufa na hakuna ndege anayeruka kwa mbawa zake hewani, isipokuwa ametutajia elimu fulani juu yake.”[7]

Imekuja kwa at-Twabaraaniy:

“Hakukubaki kitu kinachokukurubisheni na Pepo na kinakuwekeni mbali na Moto, isipokuwa kimebainishwa kwenu.”

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah hajapatapo kumtuma Mtume yeyote isipokuwa ilikuwa ni haki juu yake kuwajulisha Ummah wake ya kheri anayojua juu yao na kuwakataza ya shari anayoyajua juu yao.”[8]

al-´Irbaadhw bin Saariyah amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimekuacheni katika weupe; usiku wake ni kama mchana wake. Hakuna anayepotea isipokuwa yule anayestahiki maangamivu.”[9]

Abu-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutokea kipindi ambapo tulikuwa tunazungumzia umasikini na tunauogopa ambapo akasema: “Mnaogopa umasikini?” Naapa kwa Ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake! Dunia itamiminwa juu yenu kiasi cha kwamba hakuna kitachopotosha moyo wa mmoja wenu isipokuwa hicho.Naapa kwa Allaah! Nimekuacheni katika mfano wa weupe; usiku na usiku wake ni sawasawa.”[10]

at-Twabaraaniy amepokea kuwa Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufa na hakuna ndege anayeruka kwa mbawa zake hewani, isipokuwa ametutajia elimu fulani juu yake.”

[1] 5:3

[2] 05:03 al-I´tiswaam.

[3] 4:69

[4] 72:23

[5] 7:157

[6] 42:52-53

[7] Ahmad (5/153), al-Bazzaar (3897) na at-Twabaraaniy (1647).

[8] Muslim (1844).

[9] Ahmad (4/126), Ibn Maajah (43) na al-Haakim (1/95).

[10] Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (5).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 44-46
  • Imechapishwa: 17/05/2023