36. Watenda wenye matumbo makubwa

200 – Haaruun bin ´Abdillaah ametuhadithia: Abu Yahyaa al-Himaaniy ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Waliyd, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Ubaydillaah bin ´Umar, ambaye amesimulia kuwa ´Umar bin al-Khattwaab amesema:

”Msizunguke kwenye meza za vyakula, msije kughafilika na maakulati yote; mara nyama, mara siagi, mara mafuta na mara chumvi.”

201 – al-Mufadhwdhal bin Ghassaan amenihadithia, kutoka kwa Sufyaan bin ´Uyaynah, ambaye ameeleza kuwa ´Aliy bin Abiy Twaalib (Rahimahu Allaah) amesema:

”Mtu hawi ni mwenye kuisimamia familia yake mpaka aache kujali jinsi anavyotuliza njaa yake au namna anavyovaa.”

202 – Abu ´Aliy al-Marwaziy amenihadithia: ´Abdaan bin ´Uthmaan ametukhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha: Ibraahiym bin Nashiytw ametukhabarisha: Bwana mmoja amenihadithia:

”Jopo la watu liliingia kwa ´Abdullaah bin al-Haarith bin Jaz’ az-Zubaydiy – swahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – na wakamsikia akisema: ”Pepo iwe kwa mja ambaye wakati wa jioni anashikamana na kichwa cha farasi wake kwa ajili ya njia ya Allaah na anafungua swawm yake kwa kipande cha mkate na maji ya baridi. Maangamivu kwa wabwetekaji ambao wanabweteka kama ng´ombe na kusema ”Inua hiki, ee mfanyikazi! Weka hiki, ee mfanyikazi!” pasi na kumtaja Allaah.

203 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Zayd bin al-Habbaab ametuhadithia: Yahyaa bin al-´Alaa’ ar-Raaziy ametuhadithia: ´Abdul-Malik bin Muslim al-Lakhmiy amenihadithia, kutoka kwa baba yake, ambaye ameeleza kuwa ´Umar bin al-Khattwaab amesema:

”Naitahadharisha nafsi yangu mwenyewe [tupu], kama ´nipe, nipe, nipe tamtam, nipe chungu, nipe kilichopashwa, nipe chenye baridi”. Ni mzigo katika maisha na dhambi baada ya kifo.”

204 – Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: ´Ammaar bin ´Uthmaan al-Halabiy ametuhadithia: Muhammad bin Thaabit al-´Abdiy ametuhadithia, kutoka kwa Abu ´Imraan al-Juuniy, ambaye amesema:

”Mtu mmoja alimpa ´Aaishah uji wa ngano wa ´Iraaq. Wakati ulipowekwa mbele yake, akasema: ”Nini hii?” Wakasema: ”Ni kitu kinachotengenezwa ´Iraaq. Ni kizuri kwa kusaga chakula.” Akaanza kulia na kusema: ”Naapa kwa Allaah! Sijashiba chakula tangu alipofariki kipenzi changu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

205 – Muhammad ametuhadithia: Bahluul bin al-Muwarriq ametuhadithia, kutoka kwa Bishr bin Mansuur, kutoka kwa Thawr, kutoka kwa Khaalid bin Ma´daan, ambaye amesema:

”Nimesoma kwenye kitabu: ”Ifanye nafsi yako kuwa na njaa na uchi, pengine moyo wako ukamuona Allaah.”

206 – Muhammad ametuhadithia: ´Ammaar bin ´Uthmaan al-Halabiy ametuhadithia: Huswayn bin al-Qaasim al-Wazzaan ametuhadithia: ´Abdul-Waahid bin Zayd amesema:

”Ni kwa nini watendaji wana matumbo makubwa? Yule anayetenda kwa ajili ya Allaah anatoshelezwa na kitu chenye kumfanya kuweza kueshi.” Nimemsikia siku moja akisema: ”Nimemuahidi Allaah ahadi ambayo kamwe sintoivunja.” Nikasema: ”Ni ipi hiyo, ee Abu ´Ubayd?” Akasema: ”Wacha, ee Huswayn!” Nikasema: ”Je, hutaki maelezo yako kwangu yawe kama mfano?” Akasema: ”Ndio.” Nikasema: ”Nieleze basi.” Akasema: ”Nimemuahidi kamwe asinione ni mwenye kula mchana mpaka nitapokutana Naye.” Wakati alipokuwa mgonjwa ndugu yake wakajitahidi ale chochote, lakini akakataa mpaka alipokufa. Allaah amrehemu!”

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 128-131
  • Imechapishwa: 30/07/2023