Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Mwenye kukaa na mtu wa Bid´ah basi hakupewa hekima.”[1]
Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Usikae na mtu wa Bid´ah, kwani hakika mimi nachelea usije kushukiwa na laana.”[2]
Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Mwenye kumpenda mtu wa Bid´ah, basi Allaah atayaharibu matendo yake na ataiondosha nuru ya Uislamu ndani ya moyo wake.”[3]
Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Mtu akikaa na mtu wa Bid´ah kwenye njia, basi shika njia nyingine.”[4]
Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Ambaye atamtukuza mtu wa Bid´ah, basi amesaidia kuubomoa Uislamu. Yule mwenye kumfanyia tabasamu mzushi, ameyadharau yale Allaah (´Azza wa Jall) aliyomteremshia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwenye kumuozesha binti yake mzushi, basi amekikata kizazi chake. Mwenye kuliandama jeneza la mzushi, hatoacha kuwa katika hasira za Allaah mpaka atakaporejea.”[5]
Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Nala na myahudi na mnaswara kuliko kula na mzushi. Natamani kuwepo kati yangu mimi na mtu wa Bid´ah pazia ya chuma.”[6]
Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:
“Allaah akijua kutoka kwa mtu kuwa anamchukia mtu wa Bid´ah, anamsamehe hata kama matendo yake yatakuwa machache. Mtu wa Sunnah hawezi kumsaidia mtu wa Bid´ah isipokuwa tu kwa unafiki. Ambaye atamgeuzia mgongo wake mtu wa Bid´ah, basi Allaah ataujaza moyo wake imani. Atakayemraddi mtu wa Bid´ah, basi Allaah atampa amani siku ya Khofu kubwa. Atayemtweza mtu wa Bid´ah, Allaah atamnyanyua Peponi kwa daraja mia moja – hivyo basi kwa ajili ya Allaah kamwe usiwe mtu wa Bid´ah!”
[1] al-Laalakaa´iy katika “as-Sunnah” (263) na (1149), Ibn Battwah katika “al-Ibaanah al-Kubraa” (439) na wengineo.
[2] al-Laalakaa´iy (262) na Ibn Battwah (441) na (451).
[3] al-Laalakaa´iy (263) na Ibn Battwah (440), Abu Nu´aym (08/103) na wengineo.
[4] Abu Nu´aym (08/103), Ibn Battwah (493) na wengineo.
[5] Abu Nu´aym (08/103).
[6] al-Laalakaa´iy (1149), Abu Nu´aym (08/103) na wengineo.
- Muhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 138-140
- Imechapishwa: 30/12/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Imaam al-Fudhwayl bin ´Iyaadhw
Ni Ibn Mas´uud bin Bishr. Imaam, kiigizo, imara na Shaykh-ul-Islaam. Abu ´Aliy at-Tamiymiy al-Yarbuu´iy al-Khuraasaaniy. Alikuwa jirani na msikiti Mtakatifu. Alizaliwa Sarmakand, akakulia Abiyward na akasafiri kwa ajili ya kutafuta elimu. Kuufah aliandika kwa Mansuur, al-A´mash, Yahyaa bin Sa´iyd al-Qattwaan, Ibn Abiy Laylaa, Ja´far as-Saadiq na wengineo. Baadhi ya waliohadithia…
In "100-300 H / 700-900 M"
35. Amekosa hekima
172 - Maalik bin Anas amesema: "Ambaye atalazimiana na Sunnah na wakasalimika naye Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha akafa, basi atakuwa pamoja na Mitume, wakweli mno, mashahidi na waja wema, hata kama atafanya upungufu katika matendo." Bishr bin al-Haarith amesema: "Uislamu ni Sunnah na…
In "Sharh-us-Sunnah - al-Barbahaariy"
121. Alama ya mwenye furaha na mla khasara
Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya Muslim kupitia kwa al-Mustawrid bin Shaddaad an-Fahriy ya kwamba alimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Dunia hii ukiilinganisha na Aakhirah ni kama mmoja wenu kuchukua kidole chake akakiweka ndani ya bahari. Atazame kitatoka na nini.” ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh)…
In "Liwazo kwa waliofikwa na misiba"