Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Mwenye kukaa na mtu wa Bid´ah basi hakupewa hekima.”[1]

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Usikae na mtu wa Bid´ah, kwani hakika mimi nachelea usije kushukiwa na laana.”[2]

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Mwenye kumpenda mtu wa Bid´ah, basi Allaah atayaharibu matendo yake na ataiondosha nuru ya Uislamu ndani ya moyo wake.”[3]

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Mtu akikaa na  mtu wa Bid´ah kwenye njia, basi shika njia nyingine.”[4]

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Ambaye atamtukuza mtu wa Bid´ah, basi amesaidia kuubomoa Uislamu. Yule mwenye kumfanyia tabasamu mzushi, ameyadharau yale Allaah (´Azza wa Jall) aliyomteremshia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwenye kumuozesha binti yake mzushi, basi amekikata kizazi chake. Mwenye kuliandama jeneza la mzushi, hatoacha kuwa katika hasira za Allaah mpaka atakaporejea.”[5]

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Nala na myahudi na mnaswara kuliko kula na mzushi. Natamani kuwepo kati yangu mimi na mtu wa Bid´ah pazia ya chuma.”[6]

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Allaah akijua kutoka kwa mtu kuwa anamchukia mtu wa Bid´ah, anamsamehe hata kama matendo yake yatakuwa machache. Mtu wa Sunnah hawezi kumsaidia mtu wa Bid´ah isipokuwa tu kwa unafiki. Ambaye atamgeuzia mgongo wake mtu wa Bid´ah, basi Allaah ataujaza moyo wake imani. Atakayemraddi mtu wa Bid´ah, basi Allaah atampa amani siku ya Khofu kubwa. Atayemtweza mtu wa Bid´ah, Allaah atamnyanyua Peponi kwa daraja mia moja – hivyo basi kwa ajili ya Allaah kamwe usiwe mtu wa Bid´ah!”

[1] al-Laalakaa´iy katika “as-Sunnah” (263) na (1149), Ibn Battwah katika “al-Ibaanah al-Kubraa” (439) na wengineo.

[2] al-Laalakaa´iy (262) na Ibn Battwah (441) na (451).

[3] al-Laalakaa´iy (263) na Ibn Battwah (440), Abu Nu´aym (08/103) na wengineo.

[4] Abu Nu´aym (08/103), Ibn Battwah (493) na wengineo.

[5] Abu Nu´aym (08/103).

[6] al-Laalakaa´iy (1149), Abu Nu´aym (08/103) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 138-140
  • Imechapishwa: 30/12/2024