26. Radd juu ya utata wa kufikia malengo kupitia shirki

Kumi na moja: Miongoni mwa shubuha zao ni baadhi yao kutumia dalili kwa kule kufikia baadhi ya malengo yao kwenye makaburi. Kama wanavosema kwamba kuna mtu fulani ameomba kwenye kaburi la fulani au aliita kwa jina la Shaykh fulani au walii fulani ambapo akafikia mahitajio yake.

Jibu ni kwamba mshirikina kufikia baadhi ya malengo yake si dalili yenye kuonyesha kufaa ile shirki aliyomo. Kile alichofikia kunaweza kuwa kumekutana na mipango na makadirio na huku akifikiria kuwa kumetokamana na maombi ya Shaykh au walii huyo kama ambavo kunaweza kuwa kunatokamna na kuvutwa polepole au kupewa mtihani. Kwa hali yoyote haifahamishi kujuzu kuombwa asiyekuwa Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan Haqiyqat-it-Tawhiyd, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 02/04/2019