35. Kubadilisha maeneo ya faradhi wakati wa kuswali Sunnah

Swali 35: Je, kumepokelewa kuhusu kubadilisha maeneo ya kuswalia Sunnah baada ya swalah yanayofahamisha juu ya kupendeza kwake?

Jibu: Hakukupokelewa Hadiyth Swahiyh kutokana na ninavojua. Lakini Ibn ´Umar na wengi katika Salaf walikuwa wakifanya hivo. Wigo wa jambo hilo ni mpana. Kumepokelewa juu yake Hadiyth dhaifu kwa Abu Daawuud (Rahimahu Allaah). Inaweza kutiliwa nguvu na kitendo cha Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) na wale Salaf waliofanya hivo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 24/08/2022