172 – Maalik bin Anas amesema:

“Ambaye atalazimiana na Sunnah na wakasalimika naye Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kisha akafa,  basi atakuwa pamoja na Mitume, wakweli mno, mashahidi na waja wema, hata kama atafanya upungufu katika matendo.”

Bishr bin al-Haarith amesema:

“Uislamu ni Sunnah na Sunnah ni Uislamu.”

Fudhwayl bin ´Iyaadhw amesema:

“Pindi ninapomuona mtu katika Ahl-us-Sunnah, nahisi ni kama kwamba nimemuona mmoja katika Maswahabah wa Allaah wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pindi ninapomuona mtu katika Ahl-ul-Bid´ah, nahisi ni kama kwamba nimemuona mmoja katika wanafiki.”

Yuunus bin ´Ubayd amesema:

“Ajabu ni kwa yule ambaye leo analingania katika Sunnah. Ajabu zaidi ni kwa yule anayeitikia na kuikubali Sunnah.”[1]

Ibn ´Awn alikuwa akisema wakati wa kukata roho mpaka alipokata roho:

“Ala ala Sunnah! Ala ala Sunnah! Na tahadharini na Bid´ah.”

 Ahmad bin Hanbal amesema:

“Mmoja katika wenzangu alifariki na akaonekana ndotoni akisema: “Mwambieni Abu ´Abdillaah: “Jilazimishe na Sunnah!”, kwani hakika kitu cha kwanza alichoniuliza Allaah ni juu ya Sunnah.””

Abul-´Aaliyah amesema:

“Mwenye kufa juu ya Sunnah katika hali ya kusitiriwa, huyo ni mkweli. Kunasemwa kwamba ushikamana na Sunnah ni kuokoka.”

 Sufyaan ath-Thawriy amesema:

“Mwenye kumtegea sikio yake mtu wa Bid´ah, basi ametoka katika ulinzi wa Allaah na ametegemezwa mwenyewe kwayo.”

Kwa maana kwa Bid´ah.”

Abu Daawuud bin Abiy Hind amesema:

“Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) alimfunulia wahy Muusa bin ´Imraan: “Usikae na Ahl-ul-Bid´ah. Ukikaa nao na kukapenyeza ndani ya moyo wako kitu katika yale wanayoyasema, Nitakutupa Motoni.””[2]

[1] Abu Nu´aym (03/21), Ibn Battwah katika “al-Ibaanah al-Kubraa” (20) na wengineo.

[2] Ibn Wadhdhwaah katika “al-Bid´ah”, uk. 49.

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 136-138
  • Imechapishwa: 30/12/2024