Ibn Baaz kuhusu kusujudu juu ya nguo, mto, miiba na kadhalika

Swali: Vipi ikiwa mtu atasujudu juu ya nguo yake?

Jibu: Haidhuru, hapana vibaya ikiwa atasujudu juu ya nguo yake.

Swali: Je, ikiwa atasujudu juu ya miiba?

Jibu: Ikiwa haiumizi, hakuna tatizo. Watu wengine wana ngozi ya paji la uso yenye ukakamavu na ikiwa haiumizi, basi hapana vibaya.

Swali: Je, inafaa kwake kuinua kichwa chake, kuondoa kitu hicho kisha arudi kwenye Sujuud?

Jibu: Ndio, ainue kichwa chake, aondoshe kile chenye kumkera, kisha aweke tena paji la uso wake chini.

Swali: Je, kusujudu juu ya mto?

Jibu: Bora zaidi kusujudu bila kitu. Ikiwa mtu hawezi kusujudu kabisa, basi asitumie mto wala kitu kingine, bali asujudu kwa ishara ikiwa hana uwezo wa kusujudu moja kwa moja.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24867/حكم-السجود-على-الثوب
  • Imechapishwa: 30/12/2024