169 – Ni katika Sunnah kutomsaidia yeyote katika kumuasi Allaah, si wale wema wala mwengine katika viumbe. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Allaah. Asipendwe yeyote kwa hilo. Badala yake mtu anatakiwa kuchukia yote hayo kwa ajili ya Allaah (Tabaarak wa Ta´ala).

170 – Inatakiwa kuamini kuwa tawbah ni lazima kwa waja na watubie kwa Allaah (´Azza wa Jall) kwa dhambi ndogo na kubwa.

171 – Asiyemshuhudilia Pepo yule aliyeshuhudiliwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi huyo ni mtu wa Bid´ah na upotevu na ni mwenye kutilia shaka yale aliyosema Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 135-136
  • Imechapishwa: 30/12/2024