33. Ukafiri kutilia shaka herufi moja ndani ya Qur-aan

162 – Bid´ah zote zilizodhihiri ni kumkufuru Allaah Mtukufu. Mwenye kuzungumza kwazo hapana shaka yoyote kuwa ni kafiri.

Ambaye anaamini Kureja na kusema kwamba ´Aliy bin Abiy Twaalib, Muhammad bin ´Aliy, Ja´far bin Muhammad na Muusa bin Ja´far wako hai na watarejea kabla ya siku ya Qiyaamah, akaongea juu ya uongozi na kwamba wao wanajua ghaibu, basi tahadhari naye; kwani hakika hawa na walio na maoni haya hawamwamini Allaah Mtukufu.

163 – Twa´mah bin ´Amr na Sufyaan bin ´Uyaynah wamesema:

“Anayechukua msimamo wa kunyamaza juu ya ´Uthmaan na ´Aliy ni Shiy´iyu. Asiaminiwe, asizungumzishwe na wala mtu asiketi naye. Mwenye kumtanguliza mbele ´Aliy juu ya ´Uthmaan ni Raafidhwiy. Ameyakataa masimulizi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Yule mwenye kuwatanguliza mbele hawa watatu juu ya wengine, akawatakia rehema waliobaki na akakomeka juu ya makosa yao, yuko katika njia iliyonyooka na uongofu katika suala hili.”

164 –  Sunnah ni kushuhudia ya kwamba wale Kumi ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwashuhudia ya kuwa wako Hapana shaka yoyote juu ya hilo.

165 – Usipambanue kumtakia salamu yeyote isipokuwa tu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na familia yake.

166 – Tambua kuwa ´Uthmaan bin ´Affaan aliuawa hali ya kudhulumiwa na aliyemuua alikuwa ni mwenye kudhulumu.

167 – Mwenye kuyakubali yaliyomo ndani ya kitabu hichi, akakiamini na akakifanya kuwa ni kiigizo chema na wala asitilie shaka na kukanusha herufi yake hata moja,  basi ni mtu wa Sunnah na Mkusanyiko. Ni mkamilifu, kwa sababu Sunnah imekamilika kwake. Yule ambaye atakanusha au kutilia shaka herufi moja ya kitabu hichi au akachukua msimamo wa kukomeka, basi huyo ni mzushi.

168 – Atayekanusha au akatilia shaka herufi moja ya Qur-aan au kitu kilichotoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi atakutana na Allaah hali ya kuwa ni mkadhibishaji. Mche Allaah na utahadhari na ichunge vizuri imani yako!

  • Mhusika: Imaam Abu Muhammad al-Hasan bin Khalaf al-Barbahaariy (kfk. 329)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh-us-Sunnah, uk. 133-135
  • Imechapishwa: 30/12/2024