171 – Abu Ja´far al-Qurashiy amenihadithia: Muhammad bin Kunaasah al-Asdiy ametuhadithia:

Kila unachokula hutoka na

huongeza ladha kwenye meza ya chakula

Hubadilisha rangi baada ya kukimeza

na kinakuwa na rangi mbaya kabisa

Inapofika wakati wa kukitoa kutoka kwako,

fikiria ni utwevu kiasi gani alivyo mwanadamu

Unapokiweka mahali pake,

geuka na uzingatie mahali pale

172 – Ishaaq bin Ibraahiym ametuhadithia: ´Abdus-Swamad bin ´Abdil-Waarith ametuhadithia: Hurayth bin as-Saa-ib ametuhadithia: Nimemsikia al-Hasan akisema: Humraan amenihadithia, kutoka kwa ´Uthmaan, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mwanadamu hana haki ya kuwa na zaidi ya mambo haya: nyumba inayomsitiri, nguo inayofunika uchi wake, na mkate[1] na maji.”[2]

173 – Ismaa´iyl bin Ibraahiym bin Bassaam ametuhadithia: ´Aliy bin Thaabit ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-Hamiyd bin Ja´far, kutoka kwa ´Abdullaah bin al-Hasan, kutoka kwa mama yake, kutoka kwa Faatwimah, msichana wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Waovu katika ummah wangu ni wale waliokulia juu ya neema; wale wanaokula aina mbalimbali ya vyakula, wanavaa aina mbalimbali ya mavazi na wanazungumza kwa kujikakama.”[3]

174 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: ´Amr bin al-Haarith amenihadithia kwamba Bakr bin Sawaadah al-Judhaamiy amemuhadithia, ambaye ameeleza kuwa Hanash amemuhadithia:

”Umm Ayman alipepeta unga ili kumtengenezea mkate Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akapita karibu naye na akasema: ”Ni kitu gani hiki?” Akasema: ”Ni chakula tunachofanya katika mji wetu. Nimetaka kukufanya mkate wa bapa kwayo.” Akasema: ”Urudishe kisha ukande tena.”[4]

175 – Khaalid bin Khidaash ametuhadithia: ´Abdullaah bin Wahb ametuhadithia: ´Amr ametukhabarisha ya kwamba Bukayr bin al-Ashajj amemuhadithia:

”´Umar alimuona mtu mmoja akipepeta unga ambapo akasema: ”Uchange. Haijalengwa miti ya acacia.”

[1] at-Tirmidhiy amesema:

“Nimemsikia Abu Daawuud Sulaymaan bin Salm al-Balkhiy akisema: an-Nadhwr bin Shumayl ameema: “Yaani mkate usiokuwa na kitu cha kuweka juu.” (2341)

[2] at-Tirmidhiy (2341), aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan at-Tirmidhiy” (2341).

[3] Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ul-Jaamiy´” (3705).

[4] Ibn Maajah (3399). Cheni yake ya wapokezi ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (3399).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 112-115
  • Imechapishwa: 26/07/2023