176 – Muhammad bin Hassaan as-Samniy ametuhadithia: Ismaa´iyl bin Mujaalid ametuhadithia, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ash-Sha´biy, ambaye amesema:

”´Umar alikuwa akimwajiri mfanya kazi basi anampa sharti tatu: kusipandwe farasi wa kazi, kusivaliwe mavazi laini na wala kusipepetwe unga.”

177 – Abu ´Aliy al-Marwaziy amenihadithia: ´Abdaan bin ´Uthmaan ametukhabarisha: ´Abdullaah ametukhabarisha: Sufyaan ametuhadithia, kutoka kwa Sulaymaan, kutoka kwa Abu Waa-il, kutoka kwa Yasaar bin Numayr, ambaye amesema:

”Sijawahi hata siku moja kumpepetea unga ´Umar bin al-Khattwaab isipokuwa nilimuasi.”

178 – Abu ´Aliy al-Marwaziy amenihadithia: ´Abdaan bin ´Uthmaan ametukhabarisha: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametukhabarisha: Shu´bah ametukhabarisha, kutoka kwa Sa´d bin Ibraahiym, kutoka kwa baba yake, ambaye amesema:

”Musw´ab bin ´Umayr aliuliwa, na yeye alikuwa ni mbora kuliko mimi. Akavikwa sanda kwenye vazi lake; kinapofunikwa kichwa chake, inabaki wazi miguu yake, na inapofunikwa miguu yake, kinabaki wazi kichwa chake. Nafikiria pia kuwa alisema: ”Hamzah aliuliwa, na yeye ni mbora kuliko mimi. Kisha tukakunjuliwa katika dunia tulivyokunjuliwa. Nachelea isije kuwa malipo yetu tumeharakishiwa nayo.” Halafu baada ya hapo akaanza kulia mpaka akakiacha chakula.”

179 – Muhammad bin ´Abbaad bin Muusa ametuhadithia: Muhammad bin ´Umar ametuhadithia, kutoka kwa Ibn Abiy Dhi’b, kutoka kwa Muslim bin Jundub, kutoka kwa Nawfal bin Iyaas, ambaye ameeleza:

”Tulikuwa tumekaa na ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf. Alikuwa ni mtu mzuri wa kutangamana naye. Siku moja akatupeleka nyumbani kwake. Akatuhudumia mkate na nyama, ambapo ´Abdur-Rahmaan akaanza kulia. Tukasema: ”Ni kipi kinachokuliza, ee Abu Muhammad?” Akasema: ”Nalia kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekufa bila kushiba mkate wa shayiri.”

180 – Abu Bakr al-Baahiliy ametuhadithia: Abu ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Zaynab bint Abiy Twulayq: Hibbaan amenihadithia, kutoka kwa Abu Hurayrah, ambaye amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiunyoosha mgongo wake kwa mawe.”

181 – Ibraahiym bin Sa´iyd amenihadithia: Muusa bin Ayyuub ametuhadithia: Baqiyyah ametuhadithia, kutoka kwa Yuusuf bin Abiy Kathiyr, kutoka kwa Nuuh bin Dhakwaan, kutoka kwa al-Hasan, kutoka kwa Anas bin Maalik, kutoka kwa Mtume (Swalla Allâhu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

”Hakika miongoni mwa ubadhirifu ni wewe kula kila unachokitamani.”[1]

182 – Abu Bakr al-Baahiliy ametuhadithia: Abu ´Aaswim ametuhadithia, kutoka kwa Zaynab bint Abiy Twulayq: Nimemsikia Hibbaan akisema: Nimemsikia Abu Hurayrah akisema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliondoka kama vile anasumbuliwa na njaa. Bwana mmoja katika Maswahabah zake na akajaza vikapu ishirini kwa tende ishirini. Akaja nazo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akampa nazo ambapo akazila.”

183 – Ahmad bin Jamiyl al-Marwaziy ametuhadithia: ´Abdullaah bin al-Mubaarak ametuhadithia: al-Awzaa´iy ametukhabarisha: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Sijali kile kinachoniondoshea njaa yangu.”[2]

184 – Muhammad bin ´Aaswim ametuhadithia: Kathiyr bin Sulaym adh-Dhwabbiy ametuhadithia, kutoka kwa Anas bin Maalik, aliyesema:

”Kamwe nyama choma haikuletwa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wala hakuwahi kubebwa na mkeka.”[3]

[1] Ibn Maajah (3415). Iliyotungwa kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah” (667).

[2] Kuna wapokezi wengi wanaokosekana katika cheni ya wapokezi kwa mujibu wa al-´Iraaqiy katika “al-Mughniy ´an Haml-il-Asfaar” (2/523).

[3] Ibn Maajah (3373). Cheni yake ya wapokezi ni dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Dhwa´iyf Sunan Ibn Maajah” (656).

  • Mhusika: Imaam Abu Bakr ´Abdullaah bin Muhammad bin Abiyd-Dunyaa
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Juu´, uk. 116-121
  • Imechapishwa: 26/07/2023