Khatari ya kufanya madhambi kwa mwendelezo

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ

“Na wale ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao, basi humdhukuru Allaah wakaomba msamaha kwa madhambi yao. Na nani anayesamehe madhambi isipokuwa Allaah? Na hawaendelei katika waliyoyafanya ilihali wanajua.” (03:135)

Bi maana hawakuendelea na maasi na dhuluma zao na huku wanajua kuwa ni maasi na dhuluma. Hapa kuna dalili juu ya kwamba kuendelea [kufanya madhambi na dhuluma] pamoja na mtu kujua ni khatari sana. Hili linahusu hata madhambi madogo. Kwa ajili hii wanachuoni wengi wamesema kuwa mtu akiendelea kufanya madhambi, hata kama yatakuwa ni madogo, yanageuka kuwa makubwa. Miongoni mwa hayo ni pamoja na yale yanayofanywa na wajinga katika watu hii leo wakati wanaponyoa ndevu. Utawaona wananyoa ndevu na wanaendelea kufanya hivo. Wanaona kufanya hivo ni kujipamba na kujiweka vizuri. Uhakika wa mambo ni jambobaya. Kila jambo la maasi hakuna kheri yoyote ndani yake. Ni baya.

Watu hawa wanaoendelea kufanya maasi haya, ijapo ni madogo, lakini kwa kule kuendelea yanageuka kuwa makubwa. Kwa sababu mtu hajali. Utamuona kila siku anapotaka kwenda sokoni au kazini, anaenda kwanza na kujitazama kwenye kio, akiona unywele umoja umeanza kuota anaharakisha kuutoa au kuunyoa. Hakuna shaka yoyote juu ya kwamba huku ni kumuasi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kunakhofiwa kwa mtu huyu juu ya dhambi hii akampeleka katika dhambi kubwa na ya khatari zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/16-17)
  • Imechapishwa: 25/07/2023